Mashabiki wa Simba waliojitokeza kwenye Tamasha la Simba Day linalofanyika Kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salam .. Klabu
ya Simba yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam ina utaratibu
wake wa kuenzi vitu vyake vya klabu kwa kuanzisha siku maalumu ambayo
wanasimba wote hukusanyika pamoja kujadiliana mambo mbalimbali.Agosti
8 ya kila mwaka huwa ndiyo siku hiyo iliyopewa jina la ‘Simba Day’,
wameichagua wao Wanasimba kama sehemu ya kumbukumbu ambapo huchagizwa na
mambo mengi ikiwemo kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka,
kubadilishana mawazo, na mwisho huchezwa mechi ambayo ndiyo huitimisha
kila kitu.
0 Comments