Kaimu
Meneja Mpango wa Kudhibiti Malaria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Renatha Mandike akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya siku moja kuhusina na
hali ya malaria Nchini.
Kiongozi
Uchunguzi na Matibabu ya Malaria Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt.
Sigsbert Mkude akielezea Mikoa yenye maambukizi ya malaria nchini wakati wa semina
ya siku moja kuhusina na hali ya malaria Nchini iliyofanyika Jijini Dar es
Salaam Agosti 23, 2017
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye semina.
Mwalimu wa Kitengo cha Udhibiti Mbu waenezao Malaria kutoka Wizara ya Afya, Dkt, Charles Dismas akielezea mada kuhusina na maambukizi ya Malaria.
Watumishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia mada mbalimbali kwenye semina hiyo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina hiyo.
Kiongozi Uchunguzi na Matibabu ya Malaria Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt. Sigsbert Mkude akizungumza na waandishi wa habari.PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-MTAZAMO NEWS
..............................
Wizara
ya Afya nchini imesema maambukizi ya ugonjwa wa malaria ambao umekuwa chanzo
cha vifo vya watu wengi yamepungua kwa asilimia kubwa ingawa bado unaongoza kwa vifo.
Taarifa
hiyo imetolewa na Dkt. Sigsbert Mkude ambaye ni Kiongozi; Uchunguzi na Matibabu
ya Malaria wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwenye
semina ya waandishi wa habari iliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Semina
hiyo ilikuwa na lengo la kuelezea hali ya malaria nchini tangu mwaka 2015 hadi
2020 ambapo Dkt Mkude alisema kwa kiasi kikubwa wizara imefanikiwa kushusha
chini takwimu za maambukizi ambapo hivi sasa yamefikia asilimia 50.
Akielezea
mpango mkakati wa wizara kupambana na maradhi hayo, Mkude alisema wameona kupungua
kwa maambukizi na vifo.
Akielezea
muamko wa jamii katika upimaji wa malaria, mkude alisema upimaji katika vituo
vya tiba imeongezeka kwani mwaka 2015 ilikuwa asilimia 60 lakini hivi sasa ni
asilimia 85.
Aliongeza
kuwa katika baadhi ya mikoa wamebaini malaria siyo miongoni mwa magonjwa kumi
yanayosababisha vifo ingawa ukichanganya mikoa yote bado unaongoza.
Aliitaja
mikoa hiyo kuwa ni ya Nyanda za Juu Kusini ya Mbeya, Iringa,Njombe, ile ya kati
ambayo ni Dodoma Manyara na ya Mikoa ya nyanda za Juu Kaskazini ya Kilimanjaro
na Arusha.
Kwa
upande wa changamoto wanazokabiliana nazo, Dkt. Mkude aliizitaja kuwa ni uhamasishaji
wa jamii kutumia vyandarua kwa matumizi lengwa badala ya kutumia kinyume chake,rasimali
na usafi wa mazingira.
Changamoto
za kitaalam, usugu wa dawa za viua wadudu ambapo wakibaini hazifanyi kazi
ipasavyo huzibadili japo huwa gharama.
Akielezea muamko wa jamii kupima malaria, Dkt.
Mkude alisema wamefanikiwa kwani mwaka 2015 idadi ya wagonjwa waliopimwa malaria
ilikuwa asilimia 60 lakini hivi sasa ni zaidi ya asilimia 86.
Akielezea
matibabu ya malaria,Dkt Mkude alisema dawa ya mseto inayotumika ni ile yenye picha ya jani na si kwamba haipo kama
inavyodaiwa na baadhi ya wauzaji wa dawa.
Aidha,
aliongeza kuwa kuna maboresho makubwa ya tiba yanayofanywa na wizara.








0 Comments