Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese
akizungumza wakati wa kampeni ya afya aliyoizindua kijiji cha Malwilo kata ya
Somagedi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri
ya wilaya ya Kishapu, Dk. Josephat Shani ambaye pia mganga mkuu wa wilaya
akizunguza wakati wa uzinduzi huo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Maguja
Daniel akitoa neno wakati wa uzinduzi huo.
Mratibu wa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) mkoa wa
Shinyanga, Haruni Kasale akizungumzia umuhimu kwa wananchi kujiuna na mfuko wa
CHF iliyoboreshwa.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Malwilo
wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya afya.
Ofisa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
wilaya ya Kishapu, Jacob akitoa ufafanuzi kuhusu mradi huo wa CHF.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese
akizungumza na wananchi katika kijiji cha Malwilo wakati wa uzinduzi wa
kamnpeni hiyo ya afya.
Wananchi wakifuatilia matukio hayo.
Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Wananchi wametakiwa kujiunga na Mfuko wa Afya
(CHF) iliyoboreshwa ili wapate huduma na kuboresha afya zao na hivyo kuweza
kushiriki shughuli mbalimbali za uzalishaji.
Wito huo ulitolewa jana na Katibu Tawala Wilaya ya
Kishapu, Shadrack Kangese wakati akizindua kampeni ya uhamasishaji shughuli za
afya wilayani hapa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo
katika kijiji cha Malwilo, Mheshimiwa Nyabaganga Taraba, Kangese aliwataka
viongozi wa serikali za vijiji kuonesha mfano kwa kujiunga na mfuko huo mapema.
Kangese pia aliwataka viongozi hao kuhamasisha kaya
zingine zijiunge ifikapo Oktoba mwaka huu wakiwemo walengwa wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Alisema huduma hiyo ni muhimu kwa wananchi
wasiojiweza na wenye kipato cha chini ambapo kwa sh. 10,000 humuwezesha
kuhudumiwa yeye na watu wengine sita katika kaya kwa mwaka mzima.
Alisema Serikali imeendelea kuboresha huduma za
afya kwa kutengeneza miundombinu, kutoa vifaa tiba na kuongeza wataalamu wa
sekta hiyo ili waweze kuhudumia wananchi kwa ufanisi.
Katibu Tawala huyo aliongeza kuwa utekelezaji wa
mradi wa CHF iliyoboreshwa ulianza rasmi Machi 2016 kwa kuimarisha mfumo wa
fedha na uoreshaji dawa na vifaa tiba.
Aidha, alisema katika wilaya hiyo ni kaya 10,756
zimeandikishwa huku lengo likiwa ni kaya 42,000 ambapo kila mwananchama anapata
kadi na matibabu mwaka mzima.
Aliwataka watumishi wa afya pamoja na changamoto
ya uchache waendelee kuhudumia wananchi kwa kufuata sheria, taratibu na
miongozo iliyopo wakati Serikali inaendelea na michakato ya kuongeza wengine.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji
wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Dk. Josephat Shani aliwataka wajawazito kuhudhuria
kliniki ili kujifungua salama.
Alisisitiza umuhimu kwa wanawake kujifungulia
katika hosptali ili kupata huduma stahiki pamoja na mtoto na kuwa katika hali
ya usalama tofaui na nyumbani.
Dk. Shani ambaye pia ni mganga mkuu wa wilaya pia
aliwataka kufuata maelekezo ya watoa huduma za afya ili kuepuka kupata matatizo
yanayoweza kutokea wakati wa kujifungua.
0 Comments