Amir na
Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Tahir Mahmood Chandhry (katikati) akifafanua
jambo juu ya Mkuatano Mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo mbele ya waandishi wa habari
unaotarajiwa kufanyika tarehe 30
September hadi 1 Oktoba, leo jijini Dar
es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi
wa Jumuiya ya hiyo Sheikh Abdurahman Muhamed Ame, Kulia ni Katibu wa
Uchapishaji wa Jumuiya hiyo, Jamil Mwanga.
Amir na
Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Tahir Mahmood
Chandhry (katikati) akisoma barua iliyotumwa na Khalifatul Masihi Mkuu wa
Jumuiya hiyo duniani Mirza Mansoor Ahmad mbele ya waandishi wa habari kuelekea
katika Mkutano Mkuu wa 48 utakaofanyika
tarehe 30 September hadi 1 Oktoba mwaka huu, leo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania
Sheikh Abdurahman Muhamed Ame. Kulia ni
Kulia ni Katibu wa Uchapishaji wa Jumuiya hiyo Jamil Mwanga.
Katibu
Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Sheikh Abdurahman
Muhamed Ame (kushoto) akielezea juu ya Mkutano wa 48 wa Jumuiya hiyo mbele ya
waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika
tarehe 30 September hadi 1 Oktoba leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya hiyo Tahir Mahmood Chandhry.
Na
Neema Mathias na Thobias Robert-MAELEZO
Jumuiya ya Waislamu wa
Ahmadiyya inatarajia kufanya mkutano mkuu wa mwaka wa 48 ut kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 1
Oktoba mwaka huu katika viwanja vya Kitonga Manispaa ya Ilala, lengo likiwa ni
kuhamasisha amani, upendo ushirikiano na kutii sheria kwa waumini wa dini zote
duniani.
Hayo yameelezwa jijini
Dar es Salaam na Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdurahman Ame alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari
ambapo alisema kauli mbiu ya mkutano huo ni, “Muislam wa kweli ni yule ambaye
watu wengine wote wako salama dhidi ya shari ya ulimi wake na mikono yake.”
Kauli mbiu hiyo
inawaasa waislam duniani kote kwamba, wana haja ya kuishi na kutenda kwa namna
ambayo watu wengine watakuwa mashahidi kwamba Islam ni dini ya amani.
“Mkutano huo siyo wa
kisiasa wala si mkutano dhidi ya madhehebu mengine duniani bali unawakumbusha
waumini wa kiislamu juu ya masuala na wajibu wao wa kidini,” alifafanua Sheikh Ame.
Aidha, alisema kuwa
jumuiya hiyo ndiyo pekee miongoni mwa jumuiya za kiislam iliyo na utaratibu wa
ukhalifa ikiongozwa na kiongozi mmoja anayesimamia
utendaji katika kila nchi duniani kote.
Hapa nchini jumuiya hii ina upekee kwani ndiyo ya mwanzo kutafsiri Qurani
tukufu kwa lugha ya Kiswahili mwaka 1953.
“Jumuiya hii imekuwa
ikifanya mikutano yake mikuu kila mwaka kwa lengo la kukumbusha misingi sahihi
ya dini tukufu ya Islam, kukuza udugu na urafiki miongoni mwa wana jumuiya na wananchi
kwa ujumla na kuhamasisha uwepo wa amani katika jamii,” alieleza Sheikh Ame.
Akiwakilisha barua ya
kiongozi mkuu wa jumuiya hiyo duniania aitwaye,Hadhrat Mirza Mansoor Ahmad, Amir
na Mbashiri Mkuu wa jumuiya hiyo hapa nchini Tahir Chandhry, aliwasilisha alieleza
kuwa washiriki hawana budi kuliombea taifa amani na kujizatiti katika kuienzi
jumuiya kwa maendeleo ya dini ya uislam
duniani kote.
“Ninawahimiza nyote
mjizatiti kutimiza masharti ya baiat zenu hususan kuienzi taasisi ya kiroho ya Khilafat-e-Ahmadiyy.
Jueni ya kwamba maendeleo ya Jamaat, kuenea kwa Islam na kupatikana kwa amani
duniani, kimsingi vinaambatana na taasisi ya Ukhalifa,” alieza Chandhry.
Aidha aliongeza kuwa,
ni wajibu kwa kila mwananchama wa jumuiya hiyo popote alipo duniani anapaswa kuonesha mapenzi, nguvu na wajibu wao katika kuchangia
maendeleo ya taifa hili na kufanya kila kinachowezekana kudhibiti madaraka yao.
“Hivi ni kama vita kila
mmoja anapaswa kuwa mzalendo katika nchi yake, kutii katiba na kufanya mambo ya maendeleo kwa
ajili ya taifa letu, kwani bila amani hakuna haki,” alieleza Chandhry.
Jumuiya ya Ahmadiyya
ilianzishwa na Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s wa Qadian India mwaka 1889,
nchini Tanzania ilisajiliwa rasmi mwaka 1934 ambapo mbali na kutoa huduma za kiroho
imekuwa mstari wa mbele kutoa huduma za kijamii pasipo kujali itikadi za wananchi.
Huduma ambazo zimekuwa
zikitolewa na jumuiya hii ni kuchimba visima
vya maji, huduma za afya pamoja na elimu ya sekondari katika Mkoa wa Dar es
Salaa na elimu ya awali na msingi katika mkoa wa Morogoro pia jumuiya hiyo ipo
katika hatua za mwisho za uanzishaji na ukamilishaji wa kituo cha radio nchini.
Jumuiya Ahmadiyya ni ya kimataifa iliyoenea katika nchi 210.
Mkutano wa mwaka huu utahudhuriwa na washiriki
kutoka nchi za nje za Kenya, Uganda, Burundi, Malawi, Msumbiji na Uingereza.



0 Comments