Random Posts

Breaking News : Serikali yasema ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu popote Duniani

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
Serikali imesema ipo tayari kugharamia matibabu ya Mbunge wa Jimbo  la Singida Mashariki  Tundu Antiphas Lissu  ambaye kwa sasa hivi yupo Jijini Nairobi kwa matibabu kufuatiwa shambulio alilolipata Septemba 7,mwaka huu Mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa Jijini Tanga na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Waziri Ummy Mwalimu alisisitiza  Serikali inasubiri kupata maombi kutoka kwa familia ya mgonjwa ikiambatana na taarifa rasmi kutoka kwa  madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi  ya mgonjwa?Serikali ipo tayari  kugharamia matibabu  zaidi ya Mhe.Lissu popote Duniani?. 

Akiwa kama Mtanzania na Mbunge,Serikali inayo wajibu wa kugharamia matibabu yake hadi apone ili aweze kuendelea na kazi ya kuwahudumia Watanzania na wana Singida Mashariki.

Serikali  inapenda kusisitiza kwamba iko tayari kuendelea kushughulikia matibabu endapo maombi ya kufanya hivyo yatawasilishwa rasmi Serikalini,ikiwemo kupata taarifa ya maendeleo ya afya yake kutoka kwa Madaktari wanaomhudumia hapo Nairobi ambayo itatakiwa kupatikana kupitia ridhaa itakayotolewa na Mhe.Lissu au Mwanafamilia wa karibu kama taratibu za Kidaktari zinavyoelekeza.

Aidha, Serikali imeshangazwa na dhana ya kuchangishana kwa ajili ya matibabu ya Mhe. Lissu, kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kutokea matapeli watakaochangisha Watanzania fedha kwa madai kwamba Mbunge huyo amekosa hela za matibabu.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto anawashukuru Madaktari wa watoa huduma wote wa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya katika kuokoa masiha ya Mhe.Lissu

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
21/9/2017

Post a Comment

0 Comments