Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India, Ajay Kaul (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wao na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo kwa pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua wagonjwa 64. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wao na Hospitali ya B.L.K ya nchini India ambapo kwa pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua wagonjwa 64. Kulia ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India Ajay Kaul.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikilliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India (hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wao na Taasisi hiyo ambapo kwa pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji wa kufungua na kufungua kifua wagonjwa 64.
Picha na JKCI
...
NA MWANDISHI WETU
MADAKTARI kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete kwa
ushirikiana na wenzao wa Hospitali ya B.L.K ya nchini India wamewafanyia wagonjwa
64 upasuaji wa moyo ambao ni wa kufungua
na bila kufungua kifua.
Kati ya hao wagonjwa
nane walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na 52 walifanyiwa upasuaji wa bila
kufungua kifua (catheterization) kwa
kutumia mtambo wa Cathlab.
Pia madaktari hao
wamepata mafunzo ya kufanya upasuaji wa milango miwili ya moyo ambapo awali huduma hiyo ilikuwa haitolewi
kwenye taasisi hiyo .
Mafunzo hayo ya siku
tano yaliyo ongozwa na wataalamu kutoka Hosipitali ya BLK ya Nchini India itasaidia
serikali kuokoa zaidi ya milioni 30 ambazo zingetumika kwaajili ya matibabu ya
mgonjwa wa moyo wenye uhitaji wa upasuaji wa milango miwili ambapo asilimia 25 ya wagonjwa wana uhitaji
huo.
Akizungumza na
Waandishi wa habari jana Dar es Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Peter kisenge alisema kupitia kambi ya siku
tano ya madaktari nane wanaotibu maradhi
ya moyo ,Wataalamu wa usingizi ,Wataalamu wa kutoa damu kwenye mapafu ,kutoka
Hosipitali ya BLK ya nchini India imesaidia kutoa mafunzo ya uwekaji na
upasuaji wa milango miwili kwenye moyo kwa wagonjwa wenye matatizo hayo ambapo
huduma hiyo itakuwa ya kwanza kutolewa hapa nchini.
Mbali na huduma hiyo
Dk Kisenge alisema tayari madaktari watatu wa taasisi hiyo wanaweza kutoa
huduma ya uwekaji wa milango miwili ya damu kwenye moyo huku Daktari mmoja akipata mafunzo ya miaka
miwili nchini india.
Kuanza kwa huduma
hiyo alisema watasaidia watoto wadogo ambao milango yao imeziba ambapo awali
walikuwa hawafanyiwi upasuaji kutokana kutokuwepo kwa ujuzi wa upasuaji wa
milango hiyo.
Alisema kwa wagonjwa
64 waliofanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo wangesafirishwa nchini india
serikali ingepoteza zaidi ya bilioni 6 .
Kwa upande wake
Daktari Bingwa Upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Hosipitali ya BLK ya
Nchini India Dk Ajay Kaul alisema wataendelea kutoa ushirikiano kwa madaktari
hapa nchini ambapo baadhi ya madaktari walioambatana nao watabaki katika
taasisi hiyo kwaajili ya kuendelea kutoa mafunzo zaidi.
Dk. Kaul alisema wataendelea kuonyesha ushirikiano
wa kutoa ujuzi kwa madaktari wa hapa nchini ambapo octoba mwaka huu watatoa
mafunzo ya upandikizaji wa figo,na wagonjwa wenye matatizo ya mgongo katika
Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili.



0 Comments