Mhandisi
wa Maji toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Gratius Haule
akisisitiza jambo kwa wakazi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti wakati wa sherehe za kukabidhi vyoo kwa baadhi ya wakazi hao ambavyo
vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA)
kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) mapema
hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
na Mwanzilishi wa Taasisi Bridge for Change Bw. Ocheck Msuva akifafanua jambo kwa wakazi wa Mtaa wa Mji
Mpya Kata ya Vingunguti (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukabidhi vyoo
kwa baadhi ya wakazi hao ambavyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji
Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge
Development Initiative (CDI) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa wakazi wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti Mzee Mbesela akiwashauri
wakazi wa mtaa huo waliobahatika kujengewa vyoo na Mamlaka ya Maji Safi na Maji
Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Cambridge
Development Initiative (CDI) kuvitunza vyoo hivyo ili viweze kuwasaidia kwa
muda mrefu.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti Bw. Rahim Gassi akitoa salamu za
shukrani kwa viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam
(DAWASA) na Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) kwa kufanikisha
mradi wa ujenzi wa vyoo katika mtaa wake.
Moja
ya choo cha kisasa kilichojengwa na Mamlaka
ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na
Taasisi ya Cambridge Development Initiative (CDI) kwa wakazi wa Mtaa wa Mji
Mpya Kata ya Vingunguti.
Mhandisi
wa Maji toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Gratius Haule
(katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa vyoo katika
Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Vingunguti, vyoo hivyo vimejengwa na Mamlaka ya Maji
Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Taasisi ya
Cambridge Development Initiative (CDI).
Picha na Eliphace Marwa -Maelezo







0 Comments