MKUU wa wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo wa kwanza kulia aliyenyoosha kidole ,akitoa maelekezo kwa mganga mfawidhi wa zahanati ya Utunge ,Emmanuel Edmond wa nne kutoka kulia ,wakati wa ziara yake ya kutembelea zahanati na vituo vya afya kufuatilia fedha za mpango wa malipo ya matokeo ya ufanisi wa kazi kwenye maeneo yao (RBF)ili kuboresha huduma .
(Picha na Mwamvua Mwinyi )
MKUU wa wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo wa kwanza kulia akizungumza jambo na kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Rufiji, Didas Asenga .
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
MKUU wa wilaya
ya Rufiji ,Juma Njwayo amewaagiza waganga wafawidhi wa zahanati na vituo vya
afya wilayani hapo ,kufuata miongozo na kusimamia fedha za mpango wa malipo ya
matokeo ya ufanisi wa kazi kwenye maeneo yao (RBF)ili kuboresha huduma za afya.
Aidha amewaasa
watumishi hao kuachana na tabia ya kuingiza siasa kwenye majukumu yao hali
inayosababisha kukwama kwa jitihada za kuleta mabadiliko katika sekta hiyo.
Njwayo
,amekemea baadhi ya wauguzi hasa wodi ya uzazi ambao wamekuwa wakiwatolea lugha
zisizoridhisha na maneno machafu akinamama wanaokwenda kujifungua.
Mkuu huyo wa
wilaya ,amemtaka na kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Rufiji Didas
Asenga,kusimamia maagizo na maelekezo hayo aliyoyatoa pamoja na
kuhakikisha afisa afya anaongeza kasi ya kuweka mazingira safi kwani maeneo
mengi hususan baadhi ya zahanati,usafi hauridhishi.
Aliyasema hayo
wakati wa ziara yake aliyoianza kutembelea vituo vya afya na
zahanati 28 zilizopo wilayani Rufiji ,kufuatilia fedha za awali zilizotolewa
katika mpango wa RBF kiasi cha sh .mil.10 kila zahanati .
Njwayo
alisema, wizara imeleta mpango huo kwa dhamira njema lakini amegundua kuna
changamoto kubwa kwa baadhi ya zahanati kushindwa kufuata maelekezo na miongozo
waliyopatiwa.
“Lipo tatizo
la kutofuata maelekezo ya mradi suala litakalosababisha kukosa fedha nyingi kwa
ajili ya mradi endapo asilimia zao hazijafikia, wanajipotezea point.”alisema
Hata hivyo
alisema,hatua inayofuata baada ya kutolewa mil.10 ni kuongezwa fedha kila
zahanati kulingana na kiwango cha malipo ya ufanisi zilizoonekana .
“Nimeanza
ziara yangu leo,na nimepitia zahanati ya Tapika ambayo katika ukaguzi
uliofanywa na maofisa wa mradi wametoa asilimia 49,Ngarambe asilimia
29,Kingupira 24,Utunge 20 na zahanati ya Chumbi imejitahidi imepata
asilimia 75”alifafanua Njwayo.
Njwayo alieleza ,atakaezembea atachukuliwa hatua kwani mradi ulipoanza walipewa
miongozo na maelekezo kama hawayafuatilii ina maana wanakiuka kwa makusudi.
Aliwataka wafanyakazi wa zahanati na vituo vya afya kujenga umoja na
ushirikiano na kamati za afya ili kamati ziache
kujisahau kushirikisha na jamii kwa kuitisha mikutano kuwaeleza
masuala ya afya na umuhimu wa bima za afya .
Akizungumzia
maadili kwa watumishi wa afya,Njwayo alisema,lazima kuheshimu wagonjwa na kutoa
kauli za staha na kuwa wasiri pasipo kutoa aibu za wagonjwa mitaani.
Alisema sio
utaratibu wa namna ya kutibia wagonjwa na kama kuna mtumishi atabainika kukiuka
hayo atamchukulia hatua za kimaadili.
Kwa upande
wake kaimu mganga mkuu wilaya ya Rufiji,Didas Asenga ,alisema amepokea maagizo
na maelekezo yote aliyopatiwa.
Anasema mpango
wa malipo kwa ufanisi umeleta matokeo chanya kwani awali zahanati nyingi
zilikuwa na miundombinu chakavu,nyingine zilikuwa hazina vyoo,uhaba wa
madawa,kukosekana vichomea taka lakini kwa sasa baada ya kupatiwa mil.10 kwa
kila zahanati imeweza kuboresha huduma hizo.
Asenga
alielezea,zipo changamoto zinazojitokeza ikiwemo baadhi ya zahanati kukosa
uelewa wa hatua za manunuzi na mahesabu .
Alisema
,kunahitajika wahasibu wasaidizi katika kila zahanati ili kusimamia fedha
zijazo na kuweka kumbukumbu kitaalamu na hatimae kuondokana na mapungufu
yaliyopo.
Asenga
alibainisha,mafunzo na elimu ya kutosha inahitajika kwa wakuu wa vituo vya afya
ili kupunguza matatizo hayo.
Nae mwenyekiti
wa kijiji cha Nyamwage ,Ibrahim Said alisema mpango huo ni mzuri kwakuwa
umeweza kuimarisha huduma ya afya kwa jamii.



0 Comments