QS Albert munuo. Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) akisoma taarifa wakati akifungua Warsha ya wadau wa majengo Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa
na UDBS kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Dkt, Tumsifu Elly akiwakilisha mada yake wakati wa warsha ya wadau wa majengo Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa na UDBS kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Muhadhiri Msaidizi kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw Abdallah Katunzi akielezea Malengo ya mpango
mkakati wa kimawasiliano wakati wa warsha ya wadau wa majengo Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa na UDBS kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Muhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi Sophia Ndimbalema akitoa kuhusina na Malengo ya mpango
mkakati wa kimawasiliano.
Mkaguzi wa ndani (AQRB), Bw Ezekiel Stephen akiwakilisha mada yake.
Mwanasheria wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bw Ibrahimu Mohamed akielezea malengo mkakati wa mawasiliano ya Bodi hiyo.
Wadau mbalimbali wa majengo wakifuatili kwaumakini mada katika warsha ya Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa na UDBS kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Warsha ikiendelea.
Wadau wa majengo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa warsha ya Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa na UDBS kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es Salaam.
1.0 Maelezo kuhusu Bodi
Bodi
ya Usajili wa Wabunifu Majengo Wakadiriaji Majenzi ni taasisi ya Serikali
ambayo imeanzishwa kwa sheria Na. 4 ya mwaka 2010, na iko chini ya Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano.
Majukumu ya Bodi ni pamoja na kusaji na kudhibiti
mienendo ya Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi, Wataalamu wanaoshabihiana
nao na makampuni yao.
Pia kukuza uelewa na kuelimisha jamii kuhusu taaluma za
Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi ikiwemo kazi na wajibu wa Wabunifu
Majengo na Wakadiriaji Majenzi.
Lengo
la mkutano ni kuwashirikisha wadau wa Bodi katika mchakato wa kuandaa mkakati
wa mawasilano wa bodi, kwa kuzingatia uzoefu wao katika mada husika.
2.0 Majukumu ya Mkakati wa Mawasiliano
Jukumu
la mkakati wa mawasiliano ni kuhamasisha na kushirikishana mawasiliano kuhusu majukumu ya Bodi na wadau
katika sekta ya ujenzi.
Aidha mkakati wa mawasiliano unalenga kuelemisha jamii
kuhusu majukumu ya Bodi, wabunifu majengo, wakadiriaji majenzi na wataalum wanaoshabihiana
nao.
Kwa sasa sehemu kubwa ya jamii haitofautishi wabunifu majengo,
wakadiriaji majenzi na wahandisi; wote wanatambulika kama wahandisi Hii sio
sahihi kwa sababu kila taaluma inajitegemea, ingawa wote wanafanya majukumu yao
katika sekta ya ujenzi.
Matokeo yake ni jamii kutothamini umuhimu ya huduma za
ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi;hali inayofanya miradi yao kutokuwa na
ubora na thamani iliyokusudiwa.
Aidha mkakati wa mawasiliano utasaidia jamii kufahamu
maono , mkakati, majukumu na mafanikio ya Bodi.
2.0 Mtaalamu
Mshauri
Bodi imekuwa inawasiliana na wadau kwa njia mbali
mbali, ikiwa ni pamoja na semina,
makongamano, tovuti, vyombo vya habari. Hata hivyo Bodi imeamua kufanyike
utafiti ili kuboresha zaidi mfumo wa mawasiliano na wadau wake.
Bodi imeteua Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Kitengo cha
Biashara kutayarisha mkakati wa mawasilaino wa Bodi ili kuhamasisha kufahamika na wadau wake kwa Bodi katika sekta ya ujenzi.
Wadau ambao wamekaribishwa wanatoka serikali kuu,
serikali za mitaa, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, vyama vya taaluma
mbali mbali, Bodi za usajil, vyuo vikuu, makampuni ya ubunifu majengo na
wakadiriaji majenzi na vyombo vya habari

0 Comments