Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)
akiangalia baadhi ya picha za Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita
nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele
kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akionyeshwa ramani iliyotumika wakati wa Ukombozi
nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele
kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia)
akiangalia bango linaloelezea kumbukumbu za Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita
nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele
kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)
akiangalia mchanga wa makaburi yaliyofukuliwa ya Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita
nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele
kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)
akiangalia moja ya silaha za kivita iliyotumiwa na Mashujaa wa Tanzania wakati wa Vita vya Ukombozi
nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele
kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
Na Benedict
Liwenga-WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe amelipongeza Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuhifadhi
vema kumbukumbu za Mashujaa wa Tanzania waliopigana vita na kusaidia ukombozi
katika baadhi ya nchi za jirani ikiwemo nchi ya Msumbiji.
Pongezi hizo amezitoa leo Mkoani Mtwara wakati alipotembelea maeneo
ya kumbukumbu ya Kitaifa ambapo kwa Mkoani hapo ametembelea eneo la Mashujaa
lililopo Nailendele lengo likiwa ni kujionea maeneo yaliyoweza kuhifadhiwa
kumbukumbu zake za ukumbozi wa Bara la Afrika ikiwemo mahitaji ya ziada ya
maeneo hayo.
Mhe. Mwakyembe amesema kwamba, kazi kubwa inayofanyika katika
kuyatembelea maeneo hayo ni kujua kumbukumbu za maeneo hayo ikiwemo kuongea na
mashuhuda wa matukio ya kumbukumu za maeneo husika kwa ajili ya kuandika
historia ya Afrika kwa ushahidi uliotafutwa na Waafrika wenyewe.
“Tunakipinid kifupi kuhakikisha kuwa kumbukumbu zote tuizonazo
tunazihifadhi, tunaandika historia yetu sisi wenyewe Waafrika badala ya
kuandikiwa na Waliotutawala huko nyuma kwa ushahidi tulioutafuta wenyewe”,
alisema Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa JWTZ imefanya kazi kubwa ya kuhifadhi baadhi
ya maeneo ya kumbukumbu za kitaifa, jambo ambalo litarahisisha utunzaji wa
kumbukumbu hizo kwa ajili ya Mradi wa Ukumbozi wa Bara la Afrika.
“Tumeanza kukubaliana wote katika SADC na katika nchi za
Afrika, ni lazima tuingize katika mitaala ya shule zetu hizi harakati za
ukombozi wa Bara la Afrika ili vizazi vijavyo viweze kufahamu mambo haya
hususani tulikotoka na tunakoelekea”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha, katika ziara hiyo Mhe. Mwakyembe alipata wasaa wa
kuongea na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara ambapo ameupongeza kwa uongozi huo kwa
kuja na Mpango wa Usajili wa Vizazi vya Watoto waliopo chini ya Umri wa Miaka
Mitano ambapo Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kesho Wilayani Tandahimba.

0 Comments