Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akisalimiana na baadhi ya Viongozi
wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara kujionea
changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiongea na baadhi ya Viongozi
wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara kujionea
changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiangalia eneo la uwanja wa mpira wa miguu akiwa na baadhi ya Viongozi
wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara kujionea
changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
......
Na Benedict Liwenga-WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba pindi Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam utakapokamilia kufanyiwa ukarabati atahakikisha anapatikana
Mkandarasi Mpya mwenye vigezo na ambaye ataleta mabadiliko hususani katika
utoaji tiketi kulingana na namba za viti vilivyopo ndani ya Uwanja huo.
Kauli hiyo ameitoa jana Mkoani
Mtwara wakati alipotembelea Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Nangwanda ili kujionea
miundombinu ya uwanja huo ikiwemo baadhi ya changamoto zinazoikabili kiwanja
hicho.
Dkt. Mwakyembe ameeleza kwamba,
kumekuwa na changamoto ya kutofahamika idadi kamili ya watu wanaoingia ndani ya
uwanja hali inayopelekea watu kukaa ovyo katika sehemu zisizo rasmi na wengine
kulundikana nje ya uwanja wakati pesa za viingilio wamelipia ambapo ameweka
wazi kuwa hali hiyo inasababishwa na urataibu mbovu wa utoaji tiketi.
Akiongea na Uongozi wa Uwanja huo
wa Nangwanda Mkoani hapo alisema kwamba, kwakuwa sasa Uwanja wa Taifa uko
katika ukarabati, pindi utakapokamilika Mkandarasi mpya lazima apatikane ili
pindi mtu anunuapo tiketi yake iendane na kiti chake atakachokaa na sio
vinginevyo kwakuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuboresha sura za viwanja
nchini.
“Napenda kusisitiza suala hili
kuwa, ntahitaji apatikane Mkandarasi atakaetoa tiketi kulingana na siti
atakayokaa mtazamaji wa mpira, kwasababu kumekuwa na kero kubwa katika utoaji
tiketi hapo mwanzo jambo ambalo halileti sura nzuri kwa jamii”, alisema Dkt.
Mwakyembe.
Aliongeza kuwa Watanzania
hawanabudi kuiga mifano ya nchi nyingine ambazo zimejidhatiti katika masuala ya
utoaji tiketi wakati wa michezo.
Sambamba na hayo, Waziri
Mwakyembe ameupongeza uongozi wa uwanja huo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya
kuutunza uwanja wa Nangwanda huku akiaihidi kuzifikisha changamoto za uwanja
huo katika Viongozi wa Juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kushirikiana
kwa pamoja kuona namna ya kuzitatua.
Uwanja wa Nagwanda ulianzishwa
miaka ya 1980 ambapo awali ulikuwa ukiitwa jina la Uwanja wa Umoja Mtwara na
baadaye kupewa jina la Uwanja wa Nagwanda lililotokana na jina la mtu maarufu wakati
huo.



0 Comments