Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (kulia) akimkabidhi nahodha wa timu ya
Qatajiring zawadi mbalimbali mara baada ya kuibuka kidedea baada ya kuifunga
timu ya Zahanati wakati wa fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu. Katikati
ni mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (aliyevaa miwani) akikagua timu za
Qatajiring na timu ya Zahanati wakati wa fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani
Mbulu. Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei
Massay.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akiongea na Wananchi wakati wa kuhitimisha
fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu.
Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay akiongea
na Wananchi wakati wa kuhitimisha fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu.
Baadhi ya mashabiki
wakifuatilia fainali ya Flatei Jimbo Cup.
Baadhi ya mashabiki
wakifuatilia fainali ya Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu kati ya timu za
Qatajiring na timu Zahanati iliyochezwa katika kiwanja cha Dongobesh.
(Picha na Eleuteri
Mangi,WHUSM, Mbulu)
Na Eleuteri Mangi,
WHUSM, Mbulu
Halmashauri zote
nchini zimetakiwa kutenga maeneo ya michezo wakati wa kupanga mipango miji kwa
matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa na
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura
alipokuwa akifunga fainali ya mashindano ya Jimbo Cup inayodhaminiwa na Mbunge
wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay iliyochezwa
katika eneo la kata ya Dongobesh Wilaya ya Mbulu Mkoani wa Manyara.
“Natoa wito kwa
Halmashauri zote ikiwemo halmashauri yenu ya wilaya ya Mbulu wakati wa kupanga
matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya mipango miji mkumbuke kutenga maeneo ya
michezo, Baraza la Michezo la Taifa litatoa mafunzo ya michezo na utaalam”
alisema Naibu Waziri Wambura.
Akikabidhi zawadi za
washindi katika mashindano hayo ambao ni timu ya Qatajiring kutoka kijiji cha
tumati ambao ni mshindi wa kwanza na timu ya Zahanati kutoka kijiji cha Diomati
mshindi wa pili, Naibu Waziri Wambura amewahimiza wachezaji na wananchi
kuthamini michezo kwa kuwa ni ajira, inaleta umoja na mshikamano miongoni mwa
jamii.
Dakika 90 za fainali
hizo ziliisha kwa timu zote kufungana bao 2-2 na hatimaye timu ya Qatajiring
iliibuka kidedea kwa ifunga timu ya Zahanati kwa penati 4-1.
Akionesha umuhimu na
umahiri wa wilaya ya Mbulu katika michezo, Naibu Waziri Wambura amesema wilaya
hiyo imekuwa kitovu cha wanamichezo bora hasa mchezo wa riadha ambao wameiletea
sifa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Wanamichezo hao ni
pamoja na John Stephen Akhwari nguli mchezo wa riadha aliyeweka historia ya
kimataifa aliyewahi kusema “Nchi yangu haikunituma kuanza mashindano, ilinituma
kumaliza mashindano”Filbert Bai na wanaridha wengine.
Aidha, Naibu Waziri
Wambura amewashauri waandaaji wa mashindano hayo washirikishe pia mchezo wa
netiboli ili kuwaendeleza watoto wa kike katika mchezo huo.
Kwa upande wake
mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay amesema kuwa
alivutiwa kuanzisha mashindano hayo ili vijana wajihusishe na michezo na
kuboresha na kuendeleza afya zao na kuachana na masuala yanayoweza kupoteza
maisha yao na nguvu kazi ya taifa
Mashindano hayo
yalishirikisha timu 24 kutoka Mbulu Vijijini tangu kuanzishwa kwa mwezi Julai
mwaka huu na kufikia kilele Septemba 25 ambapo fainali ilichezwa katika viwanja
vya Dongobesh na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali na mashabiki lukuki kutoka
maeneo yote ya halmashauri hiyo.






0 Comments