Waziri wa Katiba, Sheria na Utawala Bora toka
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)
Haruna Ali Suleiman akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamed Ali
Shein katika hafla ya kufunga mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji na
Mahakimu toka nchi wananchama wa Jumiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es
Salaam.
Rais
wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola
(CMJA) Jaji John Lounders akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dkt.
Mohamed Ali Shein katika hafla ya kufunga mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha
Majaji na Mahakimu toka nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini
Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Jaji Omary Othmani
Makungu, Waziri wa Katiba, Sheria na Utawala Bora toka Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ) Haruna Ali Suleiman na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma.
Kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba, Sheria na
Utawala Bora toka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Haruna Ali
Suleiman, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.
Ibrahim Juma na Rais
wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola
(CMJA) Jaji John Lounders wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania wakati hafla
ya kufunga mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu toka nchi
wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki
wa mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu toka nchi wananchama
wa Jumuiya ya Madola (CMJA) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar
Dkt. Mohamed Ali Shein iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Katiba, Sheria na
Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Haruna Ali Suleiman leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija
- MAELEZO
.........
Na.
Paschal Dotto-MAELEZO
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema jitihada
zinazochukuliwa na serikali za nchi za Jumuiya ya Madola kuimarisha mazingira
ya kazi katika Mahakama hazina budi kwenda sambamba na kuimarika kwa utendaji
wa mahakama hizo katika kutoa huduma kwa wananchi.
Katika hotuba yake
kufunga mkutano wa siku tatu wa Chama cha Majaji na Mahakimu cha nchi wanachama
wa Jumuiya ya Madola leo, Dk. Shein amesema ni kweli kuwa Serikali ina wajibu
mkubwa katika kuimarisha mazingira ya kazi katika mahakama lakini pia mahakama
zinapaswa kutimiza wajibu wake ipasavyo.
“Majaji na Mahakimu
ni watu muhimu katika jamii kwani mmepewa nguvu kubwa na wajibu wa kipekee
katika kufanya maamuzi yanayogusa mustkabala wa pande zinazohusika katika
mashauri mnayoyaamua hivyo ni lazima wakati wote mufuate sheria na kutekeleza
majukumu yenu kwa uhuru na kwa kuzingatia maadili ya kazi yenu” alisema Dk.
Shein.
Katika hotuba yake
hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Sheria, Katiba na Utawala Bora wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Haroun Ali Suleiman, Dk. Shein alieleza kuwa
chama hicho cha Majaji na Mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola ni moja ya
taasisi zinazopigia chapuo uhuru na hadhi ya mahakama, utoaji haki na utawala
wa sheria tangu kuasisiwa kwake mwaka 1972.
Dk. Shein alitoa wito
wa ushirikiano baina ya mahakama za nchi za Jumuiya ya Madola katika
kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo vitendo vya kigaidi, usafirishaji
haramu wa binadamu, usafirishaji fedha haramu, uharamia na uvuvi haramu pamoja
na vitendo vingine hatarishi kwa maendeleo na uhai wa binadamu na kusisitiza
kuwa “Tunahitaji mahakama zenye nguvu ili kuweza kushinda vita hivi”
Aliongeza kuwa
Mkutano huo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi wanachama kwa kuwa umetoa
fursa kubwa ya kujadili changamoto zinazozikabili nchi hizo hususan katika
“mifumo yetu ya mahakama kama kucheleweshwa kwa kesi, maadili ya mahakama na
kuimarisha mazingira ya kufanyia kazi kwa maofisa wetu kwa hiyo kubadilishana
mawazo katika sehemu hizi kutaimarisha zaidi utendaji kazi”
Kwa upande wake Rais
wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ignas
Kitusi alieleza matumaini yake kuwa kutokana na mada zilizowasilishwa katika
mkutano huo, maadili ndani na nje ya mahakama yataimarika na kuleta utendaji
kazi mzuri kwa mahakama ya Tanzania.
Alibainisha kuwa
katika mkutano ujao ambao unatarajiwa kufanyika nchini Australia, washiriki
watapata fursa ya kujithmini namna walivyotekelza maazimio yaliyopitisha katika
mkutano wa Dar es salaam.
Miongoni mwa maazimio
yaliyopitishwa ni pamoja na kuyafanyia kazi maeneo mapya ya sheria ya ugaidi,
ujangili pamoja na sheria ya mtandao.




0 Comments