Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa
ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji
kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji
Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Dkt. Samson Mturi akitoa taarifa kwa
mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(hayupo pichani), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji
wa utendaji kazi wa Baraza hilo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza
jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph
Nyamhanga (kulia), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji
wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Wadau wa sekta
ya ujenzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya sekta hiyo kuhusu uboreshaji
wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mayunga Nkunya (kulia), akifafanua jambo
na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitoa
maelekezo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Bw. Milton Lupa (aliyesimama), kutoka
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa nyumba
za magomeni, jijini Dar es Salaam.
Mkadiriaji Majenzi
na Msanifu Majengo Neema Kifua (wa pili kulia), akitoa taarifa kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya
mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, alipotembelea mradi huo leo, jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya
ujenzi kuanza kuweka twakwimu takwimu zinazohusu masuala ya ujenzi hapa nchini.
Akifungua warsha ya
wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa
la Ujenzi (NCC), Prof. Mbarawa, amesisitiza umuhimu wa sekta hiyo kuimarisha
taarifa za aina, vifaa, viwango vinavyohitajika kimataifa na gharama katika
shughuli za ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, nyumba na miundombinu
mingine.
“Sekta ya Ujenzi ina
mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi na kijamii hivyo uwepo
wa taarifa mbalimbali unahitajika ili kurahisisha uelewa wa wananchi wa kawaida
katika masuala ya ujenzi na gharama zake”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha, Waziri Prof.
Mbarawa amewahakikishia wadau wa sekta ya ujenzi kuwa Serikali itaendelea
kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha sekta hiyo inakidhi matarajio ya
watanzania wengi kwa lengo la kuwajengea miundombinu iliyo bora na imara.
Ameongeza kuwa
mapendekezo yatakayotolewa na wadau hao yatarahisisha utekelezaji wa miundombiu
mbalimbali ambayo italeta chachu kwa sekta nyingine zikiwemo za kilimo,
nishati, utalii, viwanda, madini na uendelezaji wa biashara na nchi nyingine za
kikanda.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ongezeko
la miradi ya ujenzi imechangia Serikali kutafuta wataaalm waliofanya tafiti kwa
ajili ya uboreshaji wa baraza hilo wataongeza tija na ufanisi wa sekta hii
muhimu ya ujenzi kwa wadau, wananchi na Serikali.
Naye, Mwenyekiti wa
Baraza la NCC
Prof. Mayunga Nkunya amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa baraza lake
litasimamia michango yote itakayotolewa na wadau hao na kuahidi kushughulikia
changamoto zinazoikabili NCC ikiwemo za takwimu ili kuhakikisha sekta hiyo
inaendelea kukua kwa kuwa ni sekta mtambuko.
Sekta ya Ujenzi ni
mojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi hapa nchini na ina mchango mkubwa kwa Pato
la Taifa ambapo mwaka 2016 sekta hiyo ilichangia asilimia 14 ya Pato la Taifa.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 Comments