Waziri ametoa rai kwa jamii kuacha mila zinazomgandamiza mwanamke ili
kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyotokana na imani za
kishirikina. Ameiasa jamii kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuboresha
maisha yao na kutokomeza imani potofu
zinazoendeleza ukatili na mauaji ya wanawake jambo linalodhohofisha
juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa jamii zetu zinakuwa na mazingira
salama ya kuishi kwa kila Mtanzania akiwemo Mwanamke.
Mhe. Ummy Mwalimu ameitaka jamii itambue kuwa hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mtu
mwingine kitendo cha kukatisha uhai wa mtu kwa shambulio kama hili ni kosa
kisheria na Serikali itahakikisha wote wanaohusika na vitendo kama hivi, hatua
kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Kadhalika, Waziri Ummy amepongeza
Jeshi la Polisi Mkoani Tabora kwa kufika sehemu ya tukio na kuwaokoa wanawake
hao muda mfupi kabla ya jaribio la
kuteketezwa kwa moto kufuatia kuwepo kwa tuhuma za kishirikina.
Mhe. Waziri anatoa pole kwa wanawake hao pamoja
na familia zao. Aidha anawaomba kuwa na moyo wa subira na uvumilivu wakati
mamlaka zinalichunguza shauri hili.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini
Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
22/09/2017

0 Comments