Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani
Jafo akizungumza na wazee katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma wakati
akizindua Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee Tanzania Mzee
Sebastian Bulegi akitoa salamu za wazee kwa Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya
Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (hayupo Pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa Maadhimisho
ya Siku ya Wazee Duniani uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini
Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee, na Watoto Bw. Julius Mbilinyi akitoa neno kwa niaba ya Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na Watoto kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya
Siku ya Wazee Duniani uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini
Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina
Mdeme akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani
Jafo akiangalia moja ya bidhaa zilizopo katika mabanda ya maonesho ya shughuli za wazee za ujasiriamali katika
viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma kabla ya kuzindua rasmi Maadhimisho ya
Siku ya Wazee Duniani.
Baadhi ya wazee kutoka mikoa mbalimbali
Tanzania wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani
Jafo (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika viwanja vya Nyerere
Square Mjini Dodoma kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.
Baadhi ya wazee kutoka mikoa mbalimbali
Tanzania wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani
Jafo (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika viwanja vya Nyerere
Square Mjini Dodoma kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.
Kikundi cha Ngoma cha Lusombi kutoka Ruvuma kikiburudisha kwenye uzunduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee
Duniani uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani
Jafo( wa pili kushoto) akiwasili katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma kuzindua Maadhimisho
ya Siku ya Wazee Duniani kwa kuzindua maonesho ya shughuli za wazee za
ujasiriamali, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee, na Watoto Bw. Julius Mbilinyi .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani
Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya
Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kwa mwaka 2017 Mjini Dodoma
kwa kauli mbiu isemayo :“Kuelekea Uchumi
wa Viwanda:Tuthamini Mchango,Uzoefu na Ushiriki wa Wazee kwa Maendeleo ya
Taifa”
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW











0 Comments