Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ubungo John L.Kayombo amemkabidhi mkandarasi
kazi ya kujenga daraja ambalo
lilibomoka na mvua na kusababisha kero kubwa kwa wananchi wa msumi kata ya Mbezi.
Akiongea
mbele ya wananchi wa Msumi waliokuja kushuhudia
makabidhiano hayo Mkurugenzi John L.Kayombo alisema amesikia kero hii ya daraja
lililobomoka muda mrefu takribani miaka
9 iliyopita kupitia mitandao na ndipo alipoamua kufuatilia kwa ajili ya kuona
namna ya kutatua tatizo hilo ambapo baada ya kuona kero hiyo ni kubwa alichukua
maamuzi ya kughairisha mradi mwingine ili gharama za pesa ile zitumike katika
kutengeneza daraja hilo na kutatua kero hiyo kama ambavyo serikali imeahidi
kuhakikisha inatatua kero za wananchi.
Aidha
amesema kuwa katika akaunti ya kata ya mbezi kuna kiasi cha Tshs mil 100 ambazo
zitatumika kuanzia ujenzi wa daraja hilo mara moja na kuongeza kuwa kazi hiyo
inaanza mara moja wiki ijayo kwa maana ya tarehe 1/10 /2017 na itachukua muda
wa miezi 3 kukamilika.
Alimtaka
mkandarasi aliekabidhiwa kazi hiyo ambae nae alikuwepo eneo la tukio kufanya
kazi hiyo kwa uaminifu na kwa utaalamu wa hali ya juu na ndani ya muda
uliopangwa ili kuepuka matatizo yasiyo ya lazima kwani hatosita kumchukulia
hatua za kisheria pamoja na kusitisha mkataba iwapo ataenda kinyume na
taratibu.
Aliwataka
pia wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi,meneja wa TARURA na injinia ambao nao walikuwepo katika tukio hilo la
makabidhiano.
Baada
ya hapo aliwatambulisha meneja wa TARURA
kwa manispaa ya Ubungo na timu yake na mkandarasi kwa wananchi.
Nae
diwani wa kata ya mbezi Mh.Humphrey alimshukuru mkurugenzi kwa kuchukulia uzito
suala hilo na kuamua kulifanyia kazi
kero ambayo imewasumbua wananchi kwa
muda mrefu.
Nae meneja wa TARURA ndugu Laynas Sanya alimshukuru
Mkurugenzi na kuahidi kushirikiana bega kwa bega kuhakikisha kazi hiyo
inafanyika kwa ufanisi.
Mkandarasi
kampuni ya STEREO ESTATE alishukuru kwa makabidhiano hayo na kuahidi kuanza
kazi mara moja wiki ijayo na kusema atazingatia yote aliyosisitizwa na
Mkurugenzi.
Nao
wananchi waliokuwepo kwenye eneo hilo walimshukuru mkurugenzi na kusema tatizo
hilo limekuwa likiwasumbua kwa muda mrefu sasa takribani miaka 9 hivyo wana
furaha sasa kuona amelichukulia uzito na kulifanyia kazi.
Daraja
hilo litagharimu kiasi cha shilingi Mil 249,626,000 hadi kumalizika ujenzi wake
ndani ya miezi 3.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA HABARI NA MAHUSIANO- UBUNGO MUNICIPAL COUNCIL





0 Comments