Washiriki
wakiwa katika mafunzo hayo
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, Bw. Hiiti Sillo akitoa maelezo ya
utangulizi kwa washiriki
Mgeni
Rasmi, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dkt.
Ulisubisya Mpoki akisisitiza jambo katika hotuba yake ya ufunguzi
Picha
ya pamoja baina ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii ,
Jinsia , Wazee na Watoto , Dkt. Ulisubisya Mpoki (wa tatu kushoto,
msitari wa mbele), akiwa na waratibu, na washiriki wa mafunzo ya
kutathimini kwa ulinganifu ufanisi na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na
Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa
mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mali.
..........
CHUO Kikuu cha
Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili kupitia Shule ya
Famasi, kwa kushirikiana kwa Kituo cha
cha Mafunzo ya Kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki wameendesha mafunzo
ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na
Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa
mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mal.i
Akizungumza katika
ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,
Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dk. Ulisubisya Mpoki
amesema mfumo kutathimini dawa za Afrika Mashariki ni muhimu katika kuhakikisha
kuwa wananchi wa ukanda huo wanapata dawa bora, salama na zenye ufanisi mkubwa.
Dk. Mpoki amesema
mafunzo hayo ya nadharia na vitendo kwa wataalam wa dawa wa nchi za ukanda wa
Afrika Mashariki yanalenga kuhakikisha kuwa
dawa zote zilizokidhi vigezo zinasajiliwa kwa mfumo wa ulinganifu unaotumika baada wataalam hao kujiridhisha kisayansi.
Nae Mkuruenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa kumekuwa na
ushirikiano wa karibu na wananchi katika utoaji wa taarifa pale wanapoona kuna
dawa zenye mashaka ziko mtaani, hivyo kusaidia katika dhima ya kulinda afya ya
jamii.
Amesema kuwa
kuanzishwa kituo cha kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki kitakuwa ni msaada
mkubwa katika kuhakikisha kuwa kila dawa zilizo katika nchi za Afrika Mashariki
ni zilizosajiliwa na usajili kwa matumizi ya wananchi wote wa ukanda
husika.




0 Comments