Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akionyesha eneo la mradi litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (stiegler's gorge dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme.
Eneo la mradi litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (stiegler's gorge dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme,linavyoonekana
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mloka kilicho karibu na pori la akiba la Selou .(picha na Mwamvua Mwinyi )
...
Na Mwamvua Mwinyi ,Rufiji
Wakazi
wa wilaya ya Rufiji ,Mkoani Pwani pamoja na watanzania kijumla wanatarajia
kunufaika na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto
Rufiji (stiegler's gorge hydropower dam project),ambao utakuwa na uwezo wa
kuzalisha megawatts 2,100 .
Mradi
huo utazalishwa kutoka chanzo hicho , katika pori la akiba la Selou Kanda ya
Kaskazini (Matambwe ).
Kwasasa
nchi inazalisha megawatts 1,450 lakini Stiegler's gorge itazalisha megawatts
2,100 hali itakayoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi .
Akizungumza
mara baada ya kwenda kukagua na kujiridhisha eneo utakapozalishwa mradi
huo kabla ya utekelezaji kuanza,Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo,
alisema tangazo rasmi limeshatolewa na wizara ya nishati na madini tangu august
30 mwaka huu.
Aidha
alifafanua ,tangazo hilo linawapa nafasi kwa makampuni ya ujenzi wa
mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme .
Mhandisi
Ndikilo,alibainisha kampuni yoyote iwe ya ndani ama nje ya nchi ikikidhidhi
vigezo itatangazwa .
Alieleza
endapo mradi utakamilika utawezesha kuwepo kwa umeme wa uhakika na kuvutia
wawekezaji kwa wingi.
Mhandisi
Ndikilo ,alisema wilaya ya Kisarawe na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kibiti na
Rufiji umeme ukatikakatika hivyo kuna changamoto ya upungufu wa umeme
hali inayokwamisha jitihada za kuinua sekta ya uwekezaji na
viwanda .
"Tatizo
la umeme bado ni kubwa mkoani hapa licha ya mkoa huu kusheheni
viwanda "Mradi umekuja muda muafaka ambapo mkoa huo umejipanga kuwa ukanda
wa viwanda " alifafanua .
Faida
moja wapo ya mradi ni kuwa na maji mengi ya kunywa na viwandani kwa mikoa ya
Pwani ,Dar es salaam na Morogoro ,utaliii ,maji kwa ajili ya wanyama pori na
kilimo .
Mhandisi
Ndikilo alieleza ,mradi umekuja muda muafaka na umefika mahala pake ,ambapo
Mkoa huo umejipanga kuwa ukanda wa viwanda .
"Ni
nia ya serikali ya awamu ya tano kuhakikisha mawazo ya baba wa
taifa hayati mwl .Julius Nyerere ya tangu mwaka 1980 juu ya
kuzalisha umeme kutoka katika maporomoko ya mto huo yanatekelezwa kwa
haraka iwezekanavyo "alisema mhandisi Ndikilo .
Baada
ya kutembelea eneo la mradi mhandisi Ndikilo ,alipata fursa ya kwenda
kuzungumza na wakazi wa kijiji cha Mloka kilicho mpakani na pori la akiba la
Selou .
Mhandisi
Ndikilo, alisema ujenzi wa mradi huo utafungua milango ya kiuchumi na
ujasiriamali na kibiashara .
Kwa
upande wa wakazi wa Mloka ,Ikwiriri na Kibiti waliliridhia na kuonyesha
kukubali maendeleo wanayosogezewa .
Mkazi
wa Mloka ,mzee Mbonde ,alisema alikuwepo enzi za hayati baba wa taifa mradi
ulipofanyiwa tathmini na wa Norway.
Mzee
Mbonde na bibi Fatuma Majengo walimpongeza mh rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kwa kubeba mzigo .
Walisema
kwa mwanzo huu ,Dk.Magufuli atatatua tatizo la uhaba wa umeme.
Eneo
litakalotumika kujenga mradi ni kilometa za mraba 1,350 ambalo ni sawa na
asilimia tatu pekee ya eneo lote la pori la akiba la Selou yenye
ukubwa wa km za mraba 50,000 .
Mkuu
wa pori hilo la akiba la Selou kanda ya kaskazini (Matambwe)Lawrence Okode
,alisema katika historia jina la Stiegler's gorge limetokana na mjerumani
aliyefariki katika eneo hilo aliyejulikana kwa jina la Stiegler's baada ya
boti yake kugonga jiwe kubwa na kusababisha umauti wake .




0 Comments