Mkurugenzi kazi wa Shirika la REPSSI nchini
Zambia Bw. Kelvin Ngoma akitoa ufafanuzi kwa wawakilishi wa vyombo vya habari
kutoka Tanzania na nje ya nchi Jijini Arusha kuhusu nafasi ya vyombo vya habari
kuandika habari kuhusu watoto na kushawishi mabadiliko chanya ya Sera, na Programu
mbalimbali katika jamii.
Baadhi ya waandishi wa Habari kutoka
Tanzania na nje ya nchi wakimsikiliza Mkurugenzi kazi wa Shirika la REPSSI
nchini Zambia bw. Kelvin Ngoma(hayupo Pichani) akitoa ufafanuzi kwa wawakilishi
wa vyombo vya habari kutoka Tanzania na nje ya nchi Jijini Arusha kuhusu nafasi
ya vyombo vya habari kuandika habari kuhusu watoto na kushawishi mabadiliko
chanya ya Sera, Programu mbalimbali na jamii Kwa ujumla.
Mwandishi kutoka Zambia Margaret Samulela
kutoka gazeti la Daily Mail akiuliza swali kwa mwezeshaji mwelekezi kutoka
Shirika la REPSSI kuhusu masuala mablimbali ya watoto katika mkutano kati ya
shirika la REPSSI na waandishi wa habari Jijini Arusha.
Mwandishi kutoka Malawi Jacob Nankhonya
kutoka National Publications akichangia hoja kuhusu uandishi wa habari za
watoto katika mkutano kati ya shirika la REPSSI na waandishi wa habari Jijini
Arusha.
Mwandishi kutoka Lesstho Kerato Matheka
kutoka Gazeti la Public Eye akielezea jinsi chombo chao kinavyowapa nafasi
watoto katika kuelezea mambo yao na kuoigania hazi zao katika mkutano kati ya
shirika la REPSSI na waandishi wa habari Jijini Arusha.
Mtaalamu Mwelekezi kutoka Shirika la REPSSI
Bi. Carmel Gaillard akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari
kuhusu masuala ya watoto na junsi ya
kuandika na kuripoti habari kuhusu watoto katika mkutano kati ya shirika la
REPSSI na waandishi wa habari Jijini Arusha.
Picha na
KItengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW









0 Comments