Na Mwamvua
Mwinyi,Kibiti
MWENYEKITI wa ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist
Ndikilo,amewaonya waganga wa zahanati ,vituo vya afya ,ama mtumishi wa afya na
maduka binafsi ya dawa wilayani Kibiti na Rufiji kuacha kujihusisha kuwatibia
wenye majeraha yasiyoeleweka ikiwemo risasi wasiowajua bila kupata taarifa
kamili kutoka polisi .
Amesema atakaebainika
kutibia watu wa aina hiyo hatosita kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha ,mhandisi Ndikilo ,ameeleza waliokuwa wakidaiwa
kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu na mauaji wilayani humo wengi
wao wametiwa nguvuni .
Katika
hatua nyingine ,mkuu huyo wa mkoa ,amewataka wenyeviti wa Vijijini
na vitongoji kuitisha mikutano ya mapato na matumizi kuanzia sasa kwani hali ni
shwariii.
Akizungumza na wakazi wa Ikwiriri na Kibiti
,alisema matibabu yatolewe kwa mtu mwenye taarifa kutoka vyombo husika
kwani wapo baadhi ni wahalifu wanaotaka kutibiwa kinyemela.
Alisema vyombo vya
dola bado vinaendelea na mapambano ,kazi ya kudhibiti inaendelea
hadi hapo watakapojiridhisha.
Mhandisi Ndikilo,
alibainisha kwamba ,kuhusu katazo la kutumia usafiri wa pikipiki kuanzia
saa 12 jioni ,bado linaendelea ,ni marufuku usafiri huo kwa muda huo .
"Vijana wetu
madereva bodaboda najua mnategemea kipato kwenye usafiri huu lakini
tuvumilieni kidogooooo ,kidogoooo muda mdogo umebaki tutaruhusu lakini bado
Kwanzaa"
"Tunahitaji kujiridhisha kama wahalifu
waliokuwa wakiondoa amani yetu ,wamekamatwa " alisema mhandisi
Ndikilo.
Aliwasihi baadhi ya
wananchi na viongozi mbalimbali waliohama wilayani humo kwa kuogopa hali ya
sintofahamu iliyokuwepo warejee kuendelea na shughuli zao.
Alieleza kuwa ,hivi
karibuni kulikuwa na hofu na shaka kwa baadhi ya wawekezaji na wananchi kwa
hali ya usalama wao hasa katika wilaya ya Rufiji na Kibiti.
"Nami nasisitiza
kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa vyombo vya dola
vimefanikiwa kudhibiti waliokuwa wanaua ovyo,hivyo wananchi walioondoka warudi
“alisema mhandisi Ndikilo. .
Kwa mujibu wa
mwenyekiti huyo ambae pia ni mkuu wa mkoa wa Pwani,kulisitishwa mikusanyiko ya
watu ,mikutano ya hadhara ya vijiji na vitongoji lakini kwasasa iendelee .
Mhandisi Ndikilo,
alitoa wiki mbili mikutano hiyo ianze kuitishwa ,wananchi wanahitaji kujua
fedha zao zimetumiwajwe .
Nae kamanda wa kamanda
maalumu Rufiji,kamishna msaidizi mwandamizi Onesmo Lyanga,alisema wananchi
wanapaswa waelewe kilichopigwa marufuku ni kutumia usafiri wa pikipiki saa
12 jioni.
Usafiri huo
hauruhusiwi kuanzia muda huo na sio watu kuacha kuendelea na shughuli zao za
kibiashara ama kutembea.
Kamanda Lyanga
,alisema wanaendelea kushirikiana na wananchi vizuri na amewaomba endapo kuna
jambo ama viasharia vya kiuhalifu wasisitize kutoa taarifa polisi.
Aliwatoa hofu watu wote wanaofanya shughuli zao kwenye wilaya
hizo kutokuwa na wasiwasi ,ulinzi umeimarishwa .
Kamanda Lyanga
,alisema wamewashughulikia waliobainika kufanya mauaji na uhalifu katika
ukanda huo .



0 Comments