Balozi Dkt. Emmanuel J. Nchimbi akisaini
Mkataba kwaniaba ya Serikali ya Jamnhuri ya Muunganowa Tanzania wa Msamaha wa Deni
la Tanzania kwa Serikali ya Brazil .Kwa upande wa Brazil mkataba huo ulisainiwa
na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil.
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
akibadilishana mkabataba huo na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil
mara baada ya kusaini mkataba wa msamaha wa deni.
BaloziDkt. Emmanuel Nchimbi akiongoza
ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na Serikali ya Brazil.
Balozi Dkt. Nchimbi akiendelea na
mazungumzo na ujumbe wa Serikali ya Brazil (Hawapo pichani)
BaloziDkt. Emmanuel J.Nchimbi
pamoja na Mkuu wa Ujumbe wa Serikali ya Brazil Bw.Guilheme Laux
(kuliakwaBaloziNchimbi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapande zote
mbili (Tanzania na Brazil)
....
Serikali ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya Dolaza Marekani milioni
203 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania zaidi ya Bilioni 445. Deni hilo
lilitokana na mkopo uliotolewa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya
Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja Riba.
Balozi wa Tanzania Nchini Brazil Dkt. Emmanuel Nchimbi alisaini mkataba huo
kwaniaba ya Tanzania huku Wakili wa Hazina ya Taifa Dkt. Sonia Portella Nunes akisaini
kwa niaba ya Serikali ya Brazil.
Balozi Nchimbi alishukuru Serikali ya Brazil kwa Msamaha huo ambao alisema umeunga
mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli kujenga uchumi imara wa
Tanzania.
Balozi Nchimbi pia aliihakikishia Serikali ya Brazil utayari wa Tanzania
katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uchumi na Brazil.
Kiongozi wa ujumbe wa Brazil kwenye sherehe hiyo Bw. Guilheme Laux, Undersecretary of Credit and Guarantee kutoka
Wizara ya Fedha ya Brazil alimtamka rasmi kufunguliwa kwa milango ya
ushirikiano wa kifedha na kibiashara iliyokuwa imefungwa kutokana na Deni hilo
lililofanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye madeni sugu ya Brazil.
Hivyo kutoka sasa Makampuni ya Brazil yanaruhusiwa kukopa katika Benki za Brazil
kwa ajili ya kutekeleza miradi nchini Tanzania lakini pia Serikali ya Tanzania
inaruhusiwa kuanzisha majadiliano ya miradi mipya ya maendeleo.





0 Comments