Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kupokea
msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi zilizotolewa na Muungano wa Utepe
Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na
Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza
vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya na Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe
wa Uzazi Salama (WRATZ) Rose Mlay.
Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa
Uzazi Salama (WRATZ) Rose Mlay akielezea
jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi
iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye
thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni
matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya, Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kas
Medics Limited Nishitha Kulshreshtha mara
baada ya kukabidhiwa kukabidhiwa msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi
iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) kufuatia udhamini wa
kampuni hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55
ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo
Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya)
Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Pichani ni muonekano
wa mashine ya kutolea dawa za usingizi, ambayo imetolewa msaada na Muungano wa
Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye
thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni
matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini
Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija
- MAELEZO
........
Na.Paschal
Dotto-MAELEZO.
Serikali kupitia Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekabidhiwa mashine
maalumu ya kutoa dawa za usingizi kwa mama wajawazito wenye uzazi pingamizi wakati wa upasuaji kwaajili ya kuokoa maisha yao.
Akizungumza katika
makabidhiano hayo leo Jijini Dar es Salaam Waziri mwenye dhamana ya Afya Mh.Ummy
Mwalimu alisema kuwa, hiyo ni hatua kubwa katika kupambana na vifo vya wakina mama wajawazito pamoja na watoto
wachanga.
Waziri Ummy alitoa
pongezi kwa watu waliojitolea kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuunga
mkono kampeni ya kuokoa maisha ya mama na mtoto wakiongozwa na Dkt.Ahmed
Mohamed Makuwani, ambapo alisema kuwa waliopanda mlima Kilimanjaro wamewezesha
kupatikana kwa msaada wa mashine hiyo, hivyo akawashukuru na kuomba wadau
wengine kuiga mfano huo.
“Tunawashukuru Utepe
Mweupe wa Uzazi Salama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kushirikiana
na serikali ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo kwa watoto
wachanga, hatua hii inatufariji sana na naomba watanzania na wasio watanzania
wenye mapenzi mema na afya ya mama na mtoto kuendelea kusaidia juhudi hizi ”,
alisema Waziri Ummy.
Akieleza mafanikio katika
sekta ya Afya waziri Ummy alisema kuwa kuna zaidi ya vituo vya afya 480 nchi
nzima na kati ya hivyo vituo 109 vinavyumba vya upasuaji ambayo ni sawa na
asilimia 20 huku akibainisha kuwa kufikia Juni, 2018 serikali inatarajia kujenga vyumba vya upasuaji 170 vitakavyosaidia
upasuaji wa mama wenye uzazi pingamizi na idadi hiyo itaongezeka na kufikia vituo 279.
Aidha Waziri Ummy
alisema kuwa licha ya kujenga vyumba hivyo watahakikisha upatikanaji wa vifaa,
ujenzi wa maabara kubwa, wodi za kinamama pamoja na nyumba moja ya mtumishi
katika vituo vya afya vyenye vyumba vya upasuaji.
Kutokana na mpango mkakati
wa kupambana na vifo vya wajawazito na watoto
wachanga Serikali inatarajia kufikia asilimia 50 mpaka asilimia 80 ifikapo mwaka
2020 ambayo ni kampeni ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotarajia kuzinduliwa
hivi karibuni ijulikanayo kama ‘Jiongeze Tukuvushe salama’ kampeni ambayo
inalenga kuwasaidia wakina mama wajawazito popote walipo ili kuokoa maisha yao.
Naye Mratibu wa Utepe Mweupe Dkt. Rose Mlay alisema
kuwa mashine hiyo ni maalum katika kunusuru maisha ya mama na mtoto lakini pia inaweza
kutumika kwa mtu yeyote mwenye matatizo ya kufanyiwa upasuaji.
Kwa upande wake katibu
mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki
Ulisubisya alisema mashine hiyo iliyotolewa na shirika la the Guardian Health
yenye themani ya Shilingi milioni 55 ina ubora na kiwango cha kutosha katika
kutoa huduma kwa mgonjwa wakati wa upasuaji.
“Mashine hii ni ya
kipekee kwa sababu ina uwezo wa kutengeneza oksijeni na haihitaji mitungi ya
gesi kwa hiyo ni mashine nzuri kwa wagonjwa na akinamama wenye uzazi
pingamizi”, alisema Dkt.Mpoki.
Dkt. Mpoki alisema
kilichopo sasa ni kufundisha wataalam watakaohusika na matumizi ya mashine hiyo
ili waweze kuitumia ipasavyo na kuahidi kuwa atahakikisha inatunzwa ili iweze
kudumu kwa muda mrefu.





0 Comments