Mjumbe
wa Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Saum Rashid akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu
udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa, katikati ni
Bi. Angelina Mutahiwa na kulia ni Bi. Dominata Rwechungura wajumbe wa
Sekretarieti hiyo.
Mjumbe
wa Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Angelina Mutahiwa akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu
udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa, kushoto ni
Bi. Saum Rashid na kulia Bi. Dominata Rwechungura wajumbe wa Sekretarieti hiyo.
Mjumbe
wa Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Dominata Rwechungura akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu
udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa, katikati ni
Bi. Angelina Mutahiwa na kushoto ni Bi. Saum Rashid wajumbe wa Sekretarieti
hiyo.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mjumbe wa
Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Angelina Mutahiwa (aliyekaa
katikati) wakati wakitoa karipio juu udhalilishaji wa wanawake katika mitandao
kwa kisingizio cha siasa.
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
.......
Na
Thobias Robert- MAELEZO
Taasisi isiyo ya
kiserikali inayoundwa na Jumuiya za Wanawake wa Vyama vyote vya siasa (Ulingo) imelaani
vitendo vya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii vinavyofanywa na baadhi ya watu
dhidi ya viongozi wanawake wana siasa pamoja na serikali kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo Jijini
Dar es Salaam na Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Saum Rashid alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kwaaajili ya kulaani watu wanaotumia
mitandao ya kijamii kuwadhalilisha na kuwavunjia heshima viongozi wanawake.
“Matusi ambayo
wanatupiwa na watu wasio na maadili ni matusi siyo kwa wahusika tu bali kwa
wanawake wote, hivyo ikumbukwe kuwa hao wanaowalenga wanafamilia, watoto na
marafiki na wanaongoza mamilioni ya watanzania,” alifafanua Bi. Saum.
Akizungumza bila
kuwataja wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kudhalilisha viongozi, Bi.Saum
alisema wanawake wanapodhalilishwa hasa na wanawake wenzao inawakatisha tamaa
katika kutimiza majukumu yao hivyo akaomba mamlaka husika kusimamia Sheria ili
mitandao isitumike vibaya.
Aidha Bi. Saum amesema
kuwa anaamini viongozi wanawake ambao wamepewa heshima na dhamana ya kuongoza,
wana uwezo mkubwa na wanastahili kuwa kwenye nafasi walizo nazo .
Taasisi hiyo ambayo
inawashirikisha pia watu wenye ulemavu imelaani vikali vitendo vya
udhalilishaji na kuwataka watanzania warejee kwenye misingi ya utu na
kuthaminiana kama maadili ya kitanzania yanavyoelekeza hasa kwa watoto wa kike.
Kwa upande wake
Angelina Mutahiwa ambaye pia ni Mjumbe wa taasisi ya Ulingo alisema kuwa,
mwanamke ni mlezi mzuri wa maadili katika jamii hivyo kumdhalilisha ni kuvunja
malezi na maadili katika jamii na kuchochea vitendo viovu dhidi yake ambavyo
vitadumu kizazi hadi kizazi.
“Wale wachache ambao wameonesha utovu wa
nidhamu kwa kuendelea kumnyanyasa mwanamke watambue kwamba wao hawapo juu ya
sheria na katiba ya nchi iko wazi hairuhusu mwanamke kudhalilishwa, kuonewa wala
kufanyiwa vitendo vya kikatili haikubaliki na hatutakubali,” alisistiza Bi.Mutahiwa.
Ulingo ni taasisi isiyo
ya kiserikali inayoundwa na jumuiya za wanawake wa vyama vyote vya siasa
vilivyosajiliwa kwenye na Msajili wa vyama vya siasa hapa nchini kwa lengo la
kuwajengea uwezo wanawake katika nyanja mmbalimbali ili waingie kwenye vyombo
vya maamuzi.
Taasisi hiyo kwa sasa
inapigania haki sawa kwa wanawake yaani 50/50 kwani waaamini kuwa uongozi ni
haki ya kila mtu kwa maana ya wanawake na wanaume.




0 Comments