Mkurugenzi
wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bi.
Margaret Mussai akifungua kikao kazi cha Siku moja na wawakilishi kutoka
Shirika La Watoto Duniani UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya
utafiti wa vichecheo vya ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam.
Mkuu
wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Watoto katika Shirika la Umoja wa Mataifa
linalohudumia Watoto UNICEF Bi. Maud Droogleever Fortuym akitoa salamu kutoka
UNICEF wakati kikao kazi cha Siku moja na wawakilishi kutoka Shirika La Watoto
Duniani UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa vichecheo
vya ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam.
Washiriki
wa kikao kazi cha Siku moja na wawakilishi kutoka Shirika La Watoto Duniani
UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa vichecheo vya
ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam wakifuatilia jambo wakati salamu
za ufunguzi wa kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki
wa kikao kazi cha Siku moja na wawakilishi kutoka Shirika La Watoto Duniani
UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa vichecheo vya
ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam wakifuatilia jambo wakati salamu
za ufunguzi wa kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.
Na Anthony Ishengoma
Matokeo ya utafiti wa vichocheo
vya ukatili dhidi ya watoto yanaonesha bado
matendo ukatili dhidi ya watoto yamekuwa yakiongezeka kila siku hapa
Nchini kutokana na wanajamii kufanya matendo hayo bila kujua kama yana athari
kwa watoto hao.
Mkurugenzi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya
Afya, Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Margaret Mussai amesema hayo wakati wa
kikao kazi cha Siku moja na wawakailishi kutoka Shirika La Watoto Duniani
UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa vichecheo vya
ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam.
Bi. Margret Mussai amesema
utafiti huu ni mwendelezo wa utafiti wa awali wa mwaka 2009 uliotafiti kuhusu
ni namna gani mila na desturi zetu zinachangia ukatili kwa watoto hapa Nchini
ambapo matokeo ya utafiti huo ndiyo yalisababisha kufanyika utafiti mya juu ya
vichocheo vya ukatili dhidi ya watoto.
Mkurugenzi huyo amewataka Wazazi
na awalezi hapa Nchini kuwa karibu na watoto wao ili kuweza kuondoa uoga
unaowafanya watoto wao kushindwa kufanya mawasiliano ya karibu na wazazi kwani
ukatili dhidi ya watoto katika ngazi ya familia umekuwa ukifanywa na watu
wakaribu au jamaa wa wanafamilia.
Aidha Bi. Margret amesema kuwa
kariabu na mtoto, kumpenda na kumtunza mtoto hujisikia kupendwa, kuwa salama
na hivyo kujenga uwezo kujiamini na
kumweka huru kuzungumza na wazazi wake akisema kuwa mtoto anachukua mengi
kutoka kwenye jamii uku juhudi bibafsi kutoka kwenye familia kupotea kutokana
na wazazi kuwa mbali na watoto wao.
Bi. Margret pia amekemea tabia ya
baadhi ya Wananchi kukataa kutoa ushahidi mahakamani pale makosa ya ukatili
yanapowasilishwa mahakamani kwasababu watu wanofanyia watoto ukatili ni watu
walio karibu yao hivyo kitendo cha wananchi kushindwa kutoa ushaidi
kinakwamisha juhudi za serikali kupambana vitendo vya ukatili ukizingatia kuwa
haki haiwezi kutendeka bila kuwepo na ushahidi wa kutosha.
Aidha amezitaja juhudi za
serikali katika kupambana na ukatili dhidi ya watoto kuwa nikuweko kwa sheria
ya mtoto, kuwepo kwa mkakati wa kitaifa wa
kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na uwepo dawati la
mtoto katika vituo vyote vya polisi hapa Nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo
cha Ulinzi na Usalama wa Watoto katika Shirika la Umoja wa Mataifa
linalohudumia Watoto UNICEF Bi. Maud Droogleever Fortuym amesema, utafiti wa
vichocheo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto umefanywa na Chuo Kikuu
Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Huddersfield cha uingereza na
umefanyika baada ya matokeo ya awali ya utafiti wa mwaka 2009 yaliyoongalia ni
jinsi gani mila na desturi zilizopo katika jamii zinachangia vitendo vya
ukatili dhidi ya watoto.
Alibainisha
kuwa, katika utafiti huo njia zinazoangaliwa ni zile za ukatili ukiwepo ule wa
kimwili, kiakili, kutojaliwa kwa watoto pamoja na unyanyasaji na mpango wa
kwanza wa utafiti ulikuwa wa miaka mitano na ulianza 2013-2016 na sasa wako
katika mpango wa pili 2016-2021.




0 Comments