Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akimvisha taji la Miss Garden Route
2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo leo mjini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
alipokuwa akimpongeza Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo kwa ushindi wa
taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akipokea nyaraka za ushindi wa taji la
Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini kutoka kwa mshindi wa taji hilo
Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo leo mjini Dodoma.
Mshindi
wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende
Witness Teddy Kavumo.
Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.
Na Eleuteri Mangi,
WHUSM, Dodoma
Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura amewataka vijana
nchini kutumia muda vizuri na mazingira yanayowazunguka ili kufikia azma ya
malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Naibu Waziri Wambura
ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipokuwa akimpongeza Mlimbwende Witness
Teddy Kavumo ambaye ni Mtanzania anayeishi Afrika Kusini kwa kushinda taji la
Miss Garden Route 2017/2018 Mei 6 mwaka
huu nchini humo katika mji wa George.
Mlimbwnde Witness
aliibuka mshindi wa Miss Garden Route 2017/2018 akiwa ni miongoni mwa
washindani 14 walioingia fainali baada ya mchujo wa awali wa washiriki 600.
“Ni dhahiri umetumia
ujuzi, ubunifu, sanaa, imani, bidii, desturi, maadili, na sheria ambavyo
umevipata kutoka kwa familia, jamii ya
Kitanzania na pia kwa jamii ya watu wa
Afrika Kusini” amesema Naibu Waziri Wambura.
“Vijana wa
Kitanzania, Mlimbwende Witness Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017 la
Afrika Kusini amewaonesha njia, mjenge utamaduni wa kupambana na mazingira ili
kufikia azma mnazojiwekea” alisistiza Naibu Waziri Wambura.
Aidha, Naibu Waziri
huyo ameongeza kuwa Bi Witness ameonesha uzalendo kwa nchi yake kwa kuamua kuja
Dodoma na kutoa taarifa ya mafanikio yake kama Mtanzania kwa ushindi alioupata
katika mashindano ya ubunifu mavazi huko Afrika ya Kusini.
Hatua hiyo inaonesha
Mlimbwende huyo ameumeuthamini Utanzania wake na kuonesha kujali kutumia muda
wa ziada kwa masuala ya fani ya urembo licha ya kwamba jukumu lake la msingi
nchini humo ni la Kimasomo.
Zaidi ya hayo Naibu
Waziri Wambura amesema kuwa fani ya ubunifu na mitindo inatambulisha utamaduni,
kuongeza kipato, kuinua uchumi na kukuza utalii kwa kuongeza juhudi, maarifa na
kufanya kazi kwa bidii hatua nambayo inaleta matokeo mazuri yenye tija.
Aidha, Naibu Waziri
Wambura amemshauri Witness, kutumia bidhaa zenye asili ya Tanzania katika fani
yake, ili kuzitangaza katika soko la ndani na la nje, kuvutia utalii, kuingiza
kipato na kukuza uchumi katika ngazi
zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo kwake
yeye binafsi na kwa Taifa.
Kwa upande wake Miss
Garden Route 2017/2018 Mlimbwende Witness amesema kuwa anajivunia kuwa
Mtanzania na kuonesha uzalendo kwa nchi yake na amewashauri Watanzania kusimama
kwa kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao na taifa
kwa ujumla.
Mashindano ya Miss
Garden Route 2017/2018 yaliandaliwa na ‘The RoleModels Foundation” kwa
kushirikiana na Wakala wengine akiwemo “Gemini Modelling Agency” iliyopo Mossel
Bay Afrika Kusini.





0 Comments