Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana,
Ajira na wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi (aliyesimama) akizungumza na wadau
kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana alipokua
akifungua kikao cha kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa
vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James
Kajugusi (katikati) akifafanua jambo wakati wa kikao na wadau kutoka Asasi
mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana kupitia mwongozo wa Stadi
za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Ushauri Nasaha Bw. Juma
Mswadiku (kushoto) akitoa hoja wakati wa kikao na wadau kutoka Asasi mbalimbali
zinazojishughulisha na masuala ya vijana kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa
mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kupitia mwongozo
wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule wakifuatilia mada
zilizokua zikiendela leo wakati wa kikao na wadau kutoka Asasi mbalimbali
zinazojishughulisha na masuala ya vijana.
Mwezeshaji
kutoka Chama cha Stadi za Maisha (LISA) Bw. Elemeth Oloo akitoa mada kwa wadau
kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana wakati wa
kikao cha kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio
nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.
Picha
na:
Genofeva Matemu - Maelezo
Na:
Genofeva Matemu - Maelezo
Serikali
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu
imewakutanisha wadau mbalimbali kutoka Asasi zinazojishughulisha na masuala ya
vijana ili ziweze kushirikiana na serikali kupitia na kuboresha Mwongozo Sanifu
wa Stadi za Maisha kwa Vijana kwa kubadilishana uzoefu walionao na kuuwezesha
mwongozo huo kumsaidia kijana katika mazingira ya sasa.
Akifungua
kikao cha wadau hao Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na
wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi amesema kuwa msingi mkubwa wa kuboresha
mwongozi sanifu wa stadi za maisha kwa vijana ni pamoja na kuangalia namna gani
serikali inaweza kuwasaidia vijana kwa kuwawezesha kujitambua, kujiendeleza
wenyewe na kukuza uchumi wa nchi yetu.
"Mwongozo
wa stadi za maisha umekua ukiwajenga vijana kwa kuwaandaa kujitambua ili waweze
kuhimili changamoto mbalimbali zilizopo kama vile vishawishi mbalimbali vinavyowakabili,
magonjwa, matumizi ya madawa ya kulevya, mimba za utotoni pamoja na ukosefu wa
ajira" amesema Bw. Shitindi
kwa
upande wake Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi amesema
kuwa kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia, kiuchumi, kisayansi na kijamii
serikali imeona ni vyema kukaa pamoja na wadau hao kuangalia yale yaliyomo
kwenye Mwongozo wa mwaka 2009 na kufanya uchambuzi yakinifu kwa kila eneo ndani
ya mwongozo huo.
aidha
Bw. Kajugusi amewashukuru wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na
masuala ya vijana kwa kuisaidia serikali kufikisha elimu ya stadi za maisha kwa
vijana kulingana na mipango na programu zao na kuwahaidi kuendelea kufanya nao
kazi katika kujenga taifa lenye vijana wanaojitambua.
Naye
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Shirika la Kimataifa la Idadi ya watu Bibi.
Tausi Hassan ameishukuru serikali kuwakutanisha wadau wanaofanya kazi na vijana
moja kwa moja kushirikiana katika kuboresha Mwongozo wa Stadi za Maisha kwa
vijana kwani ushirikiano huo utalenga nyanja zote hivyo kupata mwongozo
unaokidhi matakwa ya vijana kitaifa.





0 Comments