Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka
mji wa Foshan China na Watazania jana Jijini Dar es Salaam. Jumla ya
wafanyabiashara 20 kuangalia fursa za uwekezaji nchini kufuatia mafanikio ya
Kiwanda cha Good One kinachotengeneza vigae. Kauli mbiu ya semina hiyo ni “Kukuza
Tanzania na Usanifu wa Makampuni”
Naibu Katibu wa Serikali ya Foshan Bw. Lai Zi
Ning akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka
mji wa Foshan China na Watanzania yenye kauli mbiu ya “Kukuza Tanzania na
Usanifu wa Makampuni” iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni wawakilishi
wa Kampuni ya Good One Bi. Winnie Mollel
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Biashara
za Kimataifa la Kamati ya Foshan China (CCPIT Foshan) Bi. DENG Xiangwen
akisisitiza jambo kuhusu nia yao ya kuwekeza nchini Tanzania wakati wa mkutano
wa wafanyabiashara kutoka mji wa Foshan China na Watanzania yenye kauli mbiu ya
“Kukuza Tanzania na Usanifu wa Makampuni” iliyofanyika jana Jijini Dar es
Salaam. Kutoka kulia ni wawakilishi wa
Kampuni ya Good One Bi. Winnie Mollel na Bi. Lillian Wu.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage akiteta jambo na Naibu Katibu wa Serikali ya Foshan Bw. Lai Zi Ning wakati
wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka mji wa Foshan China
na Watanzania iliyokuwa na kauli mbiu ya “Kukuza Tanzania na Usanifu wa
Makampuni” jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akishuhudia utiwaji saini mkataba wa
makubaliano ya kibiashara baina Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Biashara
za Kimataifa la Kamati ya Foshan China (CCPIT Foshan) Bi. DENG Xiangwen na
Meneja wa Kampuni ya Bordar Ltd Bw. Wu Yahui jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage akimkabidhi zawadi ya picha Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza
Biashara za Kimataifa la Kamati ya Foshan China (CCPIT Foshan) Bi. DENG
Xiangwen wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka mji
wa Foshan China na Watanzania iliyokuwa na kauli mbiu ya “Kukuza Tanzania na
Usanifu wa Makampuni” jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki
wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka mji wa Foshan China na Watanzania uliokuwa
na kauli mbiu ya “Kukuza Tanzania na Usanifu wa Makampuni” wakiwa katika
mkutano huo jana Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank
Shija - MAELEZO







0 Comments