Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisaini Mkataba wa Makubaliano kati
ya Tanzania na Afrika Kusini wa namna ya kutekeleza Programu ya Urithi wa
Ukombozi wa Bara la Afrika kwa lengo la kukusanya, kuhifadhi, kuendeleza na
kuzitunza urithi huo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo mjini
Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017. Kushoto ni Waziri wa Sanaa na Utamaduni,
Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akibadilishana Mkataba wa
makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika
na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika
Kusini Mhe. Nathi Mthethwa mara baada ya kusaini mkataba huo mjini Dodoma jana
Tarehe 19 Septemba 2017.
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na viongozi kutoka
Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano
wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma
jana Tarehe 19 Septemba 2017.
Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Afrika Kusini Mhe.
Nathi Mthethwa akiongea na viongozi kutoka Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria
hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi
wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitambulisha
wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano
wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma.
Waziri wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimpokea
mgeni wake Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwaalipowasili
Uwanja wa ndege mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017. Zizra hiyo inalengo
la kusaini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi
wa Bara kati ya Afrika Tanzania na Afrika Kusini.
(Picha na Eleuteri
Mangi, WHUSM, Dodoma)






0 Comments