Mwenyekiti
wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika la Alpha and Omega Reconciliation
and Peace Building (AREPEB) Yohana Mcharo (kushoto) akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki
wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, katikati ni
Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo Bi. Imelda Mushi na kulia ni
Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.
Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Alpha and
Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Bi. Imelda Mushi akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa
Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora,
kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika hilo Yohana
Mcharo na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
'''''
Na:
Thobias Robert- MAELEZO
Shirika lisilo la
kiserikali la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) limezindua mfumo wa kielektroniki wa ukuzaji
amani, haki za binadamu na misingi ya utawala bora ili kufikia maendeleo ya
Tanzania ya viwanda.
Uzinduzi huo
umefanyika Jijini Dar es Salaam leo na viongozi wa Shirika hilo katika mkutano na
waandishi wa Habari ambapo shirika limetoa namba za simu kwa lengo la kupata
maoni, ushauri pamoja na mapendekezo ya kuendeleza amani hapa nchini kwa ustawi
wa kizazi cha sasa na kijacho.
“AREPEB
inachukua fursa hii kuzindua mfumo wa kielectroniki ukataotumika kukusanya
maoni kuhusu ukuzaji amani nchini, taarifa kuhusu masuala ya haki za binadamu
na misingi ya utawala bora kwa kutumia ujumbe wa maneno kupitia namba
0800712121 au +255757333773 (ujumbe wa maneno) na +255758333773 kwa ujumbe wa
sauti na ujumbe hautakuwa na malipo,” alifafanua Bi. Angela Thadei Mwanansheria
wa Shirika hilo.
Aliendelea kusema
kuwa, mfumo huo ni huru kwa wananchi wote bila kujali, dini, itikadi za
kisiasa, ukanda au ukabila, hivyo ametoa
wito kwa wanachi kuutumia mfumo huo vizuri ili kila mwananchi aweze kuchangia
maoni yake ili kuimarisha amani nchini.
“Maoni,
ushauri na malalamiko yote yatakayotolewa ama kukusanywa, yatafanyiwa kazi na
kupata taarifa muhimu ambayo itatumika kushauri mamlaka husika, ili kuchukua
hatua kufikia matakwa ya wananchi walio wengi kuhusu kuheshimu amani
tuliyonayo, haki za binadamu na misingi ya utawala bora,” alisisitiza Bi.
Thadei.
Aidha, kupitia
ufadhili wa Foundation for Civil Society, AREPEB inatekeleza mradi wa amani
(Peace Programe), haki za binadamu na utawala bora ambao utafanyika kwa awamu
kipindi cha miezi sita kati ya mwezi
Agosti hadi Oktoba 2017 na mwaka 2018, kuanzia mwezi Februari hadi Machi.
“AREPEB inatambua
umuhimu wa kutumia vyombo vya habari kusanmbaza taarifa nchini na na kuwa ni wadau
wakubwa katika ukuzaji na ujenzi wa amani, haki za binadamu na misingi ya
utawala bora, hivyo inachukua fursa hii adimu kuviomba vyombo hivyo kushiriki
kuelimisha umma kuhusiana na program hii,” alieleza Bi. Thadei.
Aidha program
inayohusisha mafunzo ya amani na utatuzi wa migogoro pamoja na haki za binadamu
na misingi ya utawala bora inatarajiwa kuzinduliwa mkoani Pwani (Kibaha)
kuanzia tarehe 7 na 8 mwezi huu.
Aidha kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Bodi katika Mkutano Mkuu wa Shirika hilo Bw, Yohana
Mcharo alitoa wito kwa vyombo vya usalama kuendelea kulinda amani ya Wananchi
na rasilimali zao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu, lakini pia kila
mmoja kwa nafasi yake analo jukumu la
kuilinda amani na utulivu vyilivyodumu kwa muda hapa nchini.
Shirika hili
la AREPEB lilianzishwa na kusajiliwa na Serikalini mwaka 2014, kwa lengo la
kushughulikia masuala ya ukuzaji wa amani, haki za binadamu na misingi ya haki
za binadamu, utoaji wa elimu kwa umma, usuluhishi wa migogoro na kutoa mijadala
ya amani hapa nchini.


0 Comments