Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya
dawa zinavyoagizwa MSD kutoka kwa
Mfamasia wa Hospitali ya Mwananyamala Bw. Marco Sallingu kulia wakati wa ziara
yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa pili kulia akiangalia dawa ziliozopo katika
stoo za wa Hospitali ya Mwananyamala
wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es
salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya
dawa zinavyoagizwa MSD kutoka kwa Mfamasia
wa Hospitali ya Sinza Palestina Bi. Doris Messanga kulia wakati wa ziara yake
katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa katikati waliosimama akiongea na wagonjwa
wakati wa ziara yake Hospitalini Sinza
Palestina alipotembelea vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es
salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa tatu kulia akiangalia nyaraka zinazoonesha
jinsi ya dawa zinavyoagizwa MSD katika
Zahanati ya Mwenge wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya
leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza
kulia akiangalia dawa ziliozopo katika stoo za Zahanati ya Mwenge wakati
wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndungulile amefanya ziara kwenye baadhi ya vituo vitoavyo
huduma za afya kwa ajili ya kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa dawa jijini
Dar es salaam.
Akizungumza lengo la ziara hiyo Dkt. Ndungulile amesema kuwa
ameamua kufanya hivyo ili kuungana na Mhe. Rais wa awamu ya tano Dkt. John
Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kutatua tatizo la
dawa katika vituo vinavyotoa huduma za afya mpaka kufikia 2020.
?Mpaka kufikia hivi sasa katika bajeti ya mwaka wa fedha
2017/2018 Serikali imetenga shilingi Bilioni 262 kwa ajili ya kutatua tatizo la
uhaba wa dawa nchini kutoka shilingi bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/2016
? alifafanua Dkt. Ndungulile.
Aidha Dkt. Ndungulile amesema kuwa katika ziara hiyo
amegundua kwamba vituo vinavyotoa huduma ya afya vina dawa zote muhimu
isipokuwa kuna upungufu wa vifaa tiba ambapo tatizo hilo litafanyiwa kazi mara
moja .
Mbali na hayo Dkt. Ndungulile aliwataka waganga wakuu na
Wafamasia wa vituo vinavyotoa huduma za Afya kuboresha upokeaji ,utunzaji wa
dawa pindi zinapoingia kwenye stoo zao
na usimamizi mzuri wa dawa hizo.
?Vituo vinavyotoa huduma za afya lazima ziwe na kamati za
afya ambazo zitashiriki katika kupokea dawa pindi zinapotoka MSD badala yake
zinapokelewa na mtu mmoja aidha mfamasia au mtumishi mwingine wa kitengo cha
dawa? alisema Dkt. Ndungulile.
Dkt. Ndungulile leo amefanya ziara yake ya kutaka
kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa
dawa katika Hospitali ya Mwananyamala,Hospitali ya Sinza na Zahanati ya Mwenge
za jijini Dar es salaam.






0 Comments