Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro katika
maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika
mkoani humo,
Makamu Mwenyekiti wa Baraza
la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa (Mb), akielezea
mikakati ya Serikali katika kudhibiti ajali za barabarani katika maadhimisho ya
Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro,
Wanafunzi na Wananchi
wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan, katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani
kitaifa yaliyofanyika mkoani humo
Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Usalama Barabarani na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joyce Mbunju, akieleza mikakati
inayofanywa na Serikali katika kudhibiti ajali za barabarnia kwa Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipotembelea
Banda la Wizara hiyo katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani
kitaifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro
Mpima magari kutoka mzani
wa Himo, mkoani Kilimanjaro kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo
Mhandisi Adam Labay, akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipotembelea Banda la Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), katika maadhimisho ya Wiki ya nenda
kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja
na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwenye maadhimisho ya Wiki
ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiungana na kikundi cha
ngoma za asili cha Msanja, kutoka Mkoani Kilimanjaro kucheza ngoma
hiyo katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa
yaliyofanyika mkoani humo.
Madereva wa Pikipiki (bodaboda) nchini wametakiwa kutii sheria za
Usalama Barabarani bila shuruti kwani ajali nyingi zinazotokea barabarani
zimekuwa zikisababishwa na uzembe unaofanywa na madereva hao.
Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama
kitaifa mkoani Kilimanjaro Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa chanzo kikuu cha ajali hizo ni
uharaka walionao madereva hao na ukosefu wa mafunzo ya usalama barabarani kwa
baadhi ya madereva.
“Madereva wa bodaboda naomba mbadilike, muwe na tabia ya kutii
sharia za usalama barabarani bila shuruti kwani ajali nyingi nchini zimekuwa
zikisababishwa na nyinyi kutokana na haraka haraka zenu”, amesema Makamu Rais.
Aidha, amefafanua kuwa Tathmini iliyofanywa na Jeshi la Polisi
Kitengo cha Usalama Barabarani kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu
katika mkoa wa Kilimanjaro imebaini kuwa kuna ajali za Pikipiki 84
zilizojitokeza ambazo kati ya hizo, 61 zimesababisha vifo na zilizobaki
majeruhi.
Kuhusu ajali za mabasi ya abiria Mheshimiwa Makamu wa Rais amesema
kuwa zimepungua kutokana na uwepo wa mbinu za udhibiti wa mabasi hayo kama vile
upigaji picha kwa magari yanayozidisha spidi yakiwa barabarani (Tochi),
na ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa na Jeshi la polisi kupitia Kitengo
cha Usalama Barabarani katika magari ya abiria nchini.
Makamu wa Rais amefurahishwa na mkakati wa Serikali wa uandaaji wa
mfumo mpya na wa kisasa wa kuweka kamera zitakazorekodi makosa ya usalama
barabarani yanayofanywa na madereva nchini.
Ametoa rai kwa Askari wa Usalama Barabarani kutotumia kigezo cha
kupiga Tochi kwa kuwaonea, kuwanyanyasa madereva na kudai rushwa kwani vitendo
havikubaliki kisheria na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote anayejihusisha na
vitendo hivyo.
“Taswira tunayoitaka ni kuwa wananchi wawaone askari kama
walinzi wa mali zao na maisha yao na si vinginevyo”, amesisitiza Makamu wa
Rais.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amelitka Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani na wadau wake kuhakikisha wanabadilisha mbinu za namna ya
kukabiliana na tatizo la ajali nchini na kuongeza nguvu katika kudhibiti mwendo
kasi, ulevi kwa madereva, kutovaa kofia ngumu kwa waendesha bodaboda, kutofunga
mkanda kwa baadhi ya abiria na ukosefu wa vifaa vya kuwalinda watoto wadogo
wakiwa kwenye gari.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu
Nchemba (Mb), amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa wataboresha na kuunda mbinu
mbalimbali ili kudhibiti ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.
Amewataka wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali
katika kupunguza ajali za Barabarani na kuwasisitiza madereva kuzingatia sheria
za usalama Barabarani kwani hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote anayekiuka
sheria hizo.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius
Kwandikwa (Mb), amesema kuwa Baraza limekuwa likifanya jitihada mbalimbali ili
kudhibiti ajali za barabarani kama utoaji wa elimu kwa umma kupitia vyombo vya
Habari kama Televisheni na Redio pamoja na uandaaji wa viperushi na majarida.
Maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa
yaliyobeba kauli mbiu “Zuia ajali, Tii Sheria – Okoa maisha”, kwa mwaka huu
yameadhimishwa mkoani Kilimanjaro amabapo yameshirikisha wadau mbalimbali wa
usalama nchini.
0 Comments