Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri kwa kuwatema mawaziri wanne waliokuwepo kwenye baraza la awali.Mawaziri
walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu
Waziri Wizara ya Afya.
Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri Maji na
Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na
Mbunge wa Katavi, Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa
wizara hiyo.Panga hilo limempitia pia aliyekuwa Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi
yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na
nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.

0 Comments