Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu
lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoa Njombe, kwa ziara ya
kiazi ya siku moja.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwasili uwanja wa ndege
wa Njombe, kwa ziara ya kikazi ya siku moja akitokea mkoani Ruvuma, ili
kuzungumza na maafisa na askari wa Jeshi hilo pamoja na kuona changamoto
wanazokutana nazo wanapotekeleza majukumu yao na namna ya kuwasaidia.
Wajumbe
wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Njombe, wakimsikiliza Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, ambaye yupo mkoani humo kwa
ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na maafisa na
askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto wanazokutana nazo
wanapotekeleza majukumu yao na namna ya kuwasaidia.
Picha na Jeshi la
Polisi.
0 Comments