Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
33 wa Jumuiya hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mkutano huo ni
“Ardhi Kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni Chachu ya Maendeleo, Halmashauri
Zitenge Ardhi kwa Ajili ya Uwekezaji wa Viwanda Vidogo na Vikubwa”.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kassim Majaliwa akisisitiza jambo mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya
ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu
wa 33 wa Jumuiya hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mkutano huo ni
“Ardhi Kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni Chachu ya Maendeleo, Halmashauri
Zitenge Ardhi kwa Ajili ya Uwekezaji wa Viwanda Vidogo na Vikubwa”.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Suleiman Jaffo akisisitiza wakati wa
hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania
(ALAT) leo jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi Kwenye
Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni Chachu ya Maendeleo, Halmashauri Zitenge Ardhi
kwa Ajili ya Uwekezaji wa Viwanda Vidogo na Vikubwa”.
Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Shinyanga Mhe. Gullamhafeez Mukadam akisisitiza akiwasilisha salama za Jumuiya
hiyo mbele ya mgeni rasmi Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)
leo jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi Kwenye Mamlaka ya
Serikali za Mitaa ni Chachu ya Maendeleo, Halmashauri Zitenge Ardhi kwa Ajili
ya Uwekezaji wa Viwanda Vidogo na Vikubwa”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwasilisha
salama za Mkoa wake mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa
Tanzania (ALAT) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya hiyo
leo jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi Kwenye Mamlaka ya
Serikali za Mitaa ni Chachu ya Maendeleo, Halmashauri Zitenge Ardhi kwa Ajili
ya Uwekezaji wa Viwanda Vidogo na Vikubwa”.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akitazama kikundi cha ngoma alipowasili katika Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNIC) kwa ajili ya hafla ya ufunguzi
wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) leo jijini
Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi Kwenye Mamlaka ya Serikali
za Mitaa ni Chachu ya Maendeleo, Halmashauri Zitenge Ardhi kwa Ajili ya
Uwekezaji wa Viwanda Vidogo na Vikubwa”.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akitembelea mabanda ya wadau wa Tawala za Mitaa alipowasili
katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNIC) kwa ajili ya
hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania
(ALAT) leo jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi Kwenye
Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni Chachu ya Maendeleo, Halmashauri Zitenge Ardhi
kwa Ajili ya Uwekezaji wa Viwanda Vidogo na Vikubwa”.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gullamhafeez Mukadam wakati wa
hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya YA Tawala za Mitaa Tanzania
(ALAT) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Suleiman Jaffo.
Baadhi ya wajumbe wa ALAT wakifuatilia hafla ya
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa ALAT kutoka
mikoa mbalimbali baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya hiyo leo
jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi Kwenye Mamlaka ya
Serikali za Mitaa ni Chachu ya Maendeleo, Halmashauri Zitenge Ardhi kwa Ajili
ya Uwekezaji wa Viwanda Vidogo na Vikubwa”.
Picha na: Idara ya Habari - MAELEZO
....
Na.
Paschal Dotto- MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watendaji wa Serikali za Mitaa
kusimamia wananchi wao kulipa kodi ili kuimarisha huduma za jamii kwa
watanzania kwani kodi itaongeza mapato na kuboresha huduma za jamii.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa, (ALAT) Rais Magufuli amesema kuwa ili nchi iweze kuendelea kiuchumi lazima wananchi wake walipe
kodi kwani hicho ni miongoni mwa chanzo muhimu cha mapato ya Serikali
kinachoiwezesha kuwapatia wananchi huduma nzuri na bora.
“Tulianza kuimarisha
ukusanyaji wa mapato na kudhibiti ubadhirifu wa fedha za umma, tulibana mianya
ya ukwepaji kodi na kuongeza ukusanyaji mapato kutoka bilioni 800 kwa mwezi hadi
trilioni 1.3 kwa mwezi” Rais Magufuli alieleza.
Alifafanua kuwa
kutokana na ongezeko hilo Serikali sasa inaweza kulipa mishahara kwa wakati huku
ikilipa madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ilikuwa inaidai Serikali
shilingi trilioni 1.3 ambapo hadi sasa imeshalipwa shilingi trilioni 1.2.
Rais Magufuli
alieleza kuwa katika utendaji kazi wa ALAT mkutano huo ni muhimu kwa serikali anayoiongoza
kwani Jumuiya hiyo ni mhimili muhimu wa kuwaunganisha wananchi na serikali yao
hivyo mkutano huo kwa nchi yetu una
umuhimu wa kipekee.
“Kwangu mimi mkutano
huu ni muhimu sana kwa sababu ALAT ni chombo kinachounganisha mamlaka na wadau
wanaohusika na masuala ya Serikali”, alisisitiza Rais Magufuli.
Akibainisha miradi
iliyotekelezwa mpaka sasa kutokana na mapato ya wananchi, Rais Magufuli alisema
kuwa huduma ya elimu imeboreka zaidi baada ya serikali kuanza utaratibu wa kutoa
shilingi bilioni 18 kwa mwezi katika mwaka wa fedha 2015-2016.
Kufuatia hatua hiyo
alisema idadi ya watoto waliojiandikisha kuingia darasa la kwanza ilifikia
asilimia 95 huku kidato cha kwanza wanafunzi wakiongezeka kwa asilimia 30
ambapo alisisitiza kuwa uwezo huo umetokana na kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato.
Rais Magufuli aliwaambia
wajumbe wa mkutano huo kuwa katika kutekeleza mpango wa Serikali ya Awamu ya
Tano wa kuimarisha miundombinu, serikali imeshatia saini mkataba wa ujenzi wa
reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam mpaka Makutupora Dodoma, ambapo kwa awamu
ya kwanza itaanzia Dar es Salaam mpaka Morogoro.
Mradi huu mkubwa utagharimu
kiasi cha fedha za kitanzania shilingi trilioni 7.062 ambazo kwa asilimia 100
ni fedha za serikali kutoka kwa wananchi walipa kodi.
Alitaja miradi
mingine kuwa ni upanuzi wa bandari mbalimbali za mizigo zikiwemo bandari za Mtwara
bilioni 130, Dar es Salaam bilioni 926.2, Tanga bilioni 16 pamoja na ukarabati
wa meli za mizigo katika Ziwa Nyasa na Ziwa Viktoria ambapo pesa zote hizo ni za
serikali kwa asilimia 100.
Akijibu risala ya
ALAT, Rais Magufuli ameipongeza Jumuiya hiyo na kuwataka wapambane na wasiogope
katika kutenda na kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.
Naye Mwenyekiti wa ALAT,
Gulamhafeez Mukadam ameiomba Serikali kutenga na kupeleka kwa wakati ruzuku
katika Halmashauri zao ili waongeze ufanisi katika kazi ya kuwatumikia wananchi
na kwenda na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Kauli mbiu ya mkutano
huo wa 33 ni “Ardhi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ni chachu ya maendeleo,
Halmashauri zitenge ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vidogo na vikubwa”
ambapo Mukadam alisema kuwa kauli mbiu hiyo inakwenda sambamba na sera ya Serikali
ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya viwanda.
ALAT ilianzishwa 1984
kwa lengo la kuwakutanisha pamoja watendaji wa Serikali za Mitaa ili waweze
kubadilishana uzoiefu masuala ya utendaji kazi.










0 Comments