Dubai, United Arab Emirates, October 22, 2017 – TECNO, Kampuni
kubwa ya simu za mkononi TECNO iliyopo chini ya TRANSSION HOLDINGS ,
imetambulisha rasmi simu yake mpya katika harakati zake za kukuza soko
katika nchi za Asia na Africa, TECNO Phantom 8 katika jiji la Dubai.
Matumizi
ya smartphone yanakua kwa kasi katika maeneo ya nchi za kiafrika na za
mashariki ya kati kwa kiasi cha milioni 123. 7 mpaka 2016 toka milioni
106.4 mwaka 2015.
“Hivi
karibuni ripoti zinaonyesha kwa kiasi kampuni imeweza kupenya katika
soko na kuleta ushindani katika bara la Afrika na mashariki ya kati”
Alisema makamu wa rais wa kampuni mama TRANSSION HOLDINGS, Arif Chowdhury.
“Mipango yetu ni mwaka jana ilikua kukua zaidi kupitia mashariki ya
kati hivyo kuzindua rasmi Phantom 8 jiijini Dubai ni hatua mojawapo
katika kuendeleza mipango hii. Simu zetu zitaendelea kujikita katika
kufuata mahitaji ya wateja zaidi”. Alimaliza Makamu wa raisi.
TECNO
Mobile inaendelea kutoa bidhaa zenye ubora kwa wateja wake hasa barani
Africa ambapo kampuni hiyo ina nafasi kubwa katika mauzo hasa kwa nchi
kama Tanzania na Nigeria na nchi kadhaa kutokea mashariki ya kati.
Kwa
zaidi ya miaka 11 TECNO imekua ikifanya kazi ya kuunganisha wananchi
katika mawasiliano kupitia simu hasa kwa kuleta simu zenye ubora na bei
inayoendana na watumiaji wake.
Simu
hiyo iliyozinduliwa jijini Dubai imekua gumzo tangu tetesi zitoke kua
inakuja sokoni imezinduliwa ikiwa na jina la Phantom 8 huku ikiwa
imetengenezwa kwa teknolojia kubwa hasa kwa upande wa kamera ikiwa na
megapixel 20 mbele na kamera mbili nyuma6 GB RAM na ROM ikiwa ni 64GB.
Kwa upande wa dizaini simu inametengenezwa vizuri ikiwa na muundo wa
mithili ya Almasi na kioo.
Phantom 8 kutarajiwa kufika mabara mengine pia duniani.
Phantom
8 inauwezo wa kuweka “simcard” aina ya “Nano/ Micro” na inauwezo wa
kumud memory card ya hadi 2TB (Terra Bytes) na pia inauwezo wa 4G plus
ambayo inakuwezesha kutumia simu yako ndani na Zaidi ya nchi 200.
Kwa
wateja waliopo Tanzania wataweza kuagiza simu hii mpya katika maduka maalumu ya simu za TECNO ili kuweza kuipata inapoingia sokoni siku
chache zijazo.
Phantom 8 iliyozinduliwa
hivi karibuni iikiwa imesheheni na sifa za kipekee kama Kamera, Ubo na
muonekano wa kipekee pamoja na kasi ya ajabu. Kamera ikiw ana uwezo wa
20 MP, pamoja na kamera pacha zenye uwezo wa 13Mp +12 Mp kamera za nyuma
ikiambatana na uwezo wa kuvuta picha mara 10 zaidi ya kamera ya
kawaida, Ina uwezo wa HDR,4 in 1 uwezo wa kungarisha picha,AF na mambo
mengine mengi yenye kukuhahkishia kupata picha zilizo bora na zenye
muonekano mzuri.
Kwa maelezo zaidi kuhusian na TECNO Mobile tembelea https://www.tecno- mobile.com/index.php?m=Home&c= Index&a=index
###





0 Comments