Mkurugenzi Msaidizi wa
Sera na Takwimu Bwana Adamu Mwaigoga, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), akimkaribisha Naibu Waziri wa Sekta ya
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, alipowasili Wizarani mjini
Dodoma kwa mara ya kwanza.
Mmoja wa watumishi wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (wa Sekta ya Uchukuzi), Bi. Rose Mwalujuwa,
akimkaribisha Naibu Waziri wa Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye, alipowasili Wizarani mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Mhandisi
Anjelina Madete (kulia), akimkaribisha Naibu Waziri wa Sekta ya Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), Wizarani mjini Dodoma
alipowasili kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika nyadhifa hiyo na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mkurugenzi wa Idara ya
Rasilimali Watu na Utawala wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta
ya Mawasiliano), Bi. Kitolina Kippa (kulia), akimkaribisha Naibu Waziri wa
Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), Wizarani mjini Dodoma alipowasili kwa mara ya
kwanza tangu ateuliwe kushika nyadhifa hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.




0 Comments