Mhandisi Mshauri
anayesimamia ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Songwe (SIA), Eng. Nyamhanga Wanda, akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua
maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, mkoani Mbeya.
Mkandarasi anayejenga
jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), Kannan
Thiyagamoorthy, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo,
mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, (kushoto) , akikagua ujenzi wa
jengo la abiria linalojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe
(SIA), Waziri huyo alifanya ziara ya ukaguzi na kuangalia maendeleo
yaliyofikiwa ya ujenzi huo hadi sasa. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa.
Muonekano wa Jengo la
abiria linalojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA). Jengo
hilo limetakiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi Januari, 2018
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza na
wananchi wa Tunduma wakati akikagua upanuzi wa njia nne ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga
KM 1.45, mkoani Mbeya.
Meneja wa Wakala wa
Barabara (TANROADS), mkoa wa Songwe Eng. Yohane Kasaini (katikati), akitoa
maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(kulia), wakati wa ukaguzi wa upanuzi wa njia nne ya barabara ya
Tunduma-Sumbawanga KM 1.45, mkoani Mbeya.
Muonekano wa sehemu ya
barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 1.45 inayojengwa kwa njia nne, mkoani Mbeya
ili kupunguza msongamano wa magari jijini hapo.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa
mkandarasi GM Construction anayejenga jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Songwe (SIA), kukamilisha ujenzi huo.
Amesema Serikali
hairidhishwi na kasi ya ujenzi wa jengo hilo ambalo limetumia miaka minne
badala ya miwili iliyokubalika katika mkataba wa awali hivyo kumtaka mkandarasi
huyo kuhakikisha analikabidhi jengo hilo ifikapo Januari 30 mwakani.
“Kushindwa kukamilisha
jengo hili ifikapo mwezi Januari mwakani itakuwa ndio tiketi yako ya mwisho ya
kutopewa kazi kwasababu Serikali hii inafanya kazi kwa kuzingatia ubora na
muda”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa
amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng.
Paul Lyakurwa kusimamia kikamilifu ujenzi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa
wakati na kwa ubora uliokusudiwa
“Ujenzi wa miundombinu
ya viwanja vya ndege kwa sasa unasimamiwa na TANROADS na uendeshaji wake unasimamiwa
na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuongeza
kasi ya ujenzi wa viwanja vya ndege na ubora wa huduma zinazotolewa katika
viwanja hivyo”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Katika hatua nyingine
Prof. Mbarawa, amekagua upanuzi wa barabara katika mji wa Tunduma unaolenga
kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo na kuwahakikishia wananchi kuwa
ujenzi wake utakamilika mwishoni mwa mwezi ujao.
Amewataka wakazi wa
Tunduma kuilinda miundominu ya barabara hizo kwa kuzingatia matumizi sahihi ili
kuleta usalama kwa wananchi.
Naye Meneja wa
TANROADS, mkoa wa Songwe Eng. Yohane Kasaini, amemuhakikishia Waziri Prof.
Mbarawa kwamba barabara za michepuko zitaongezwa katika eneo la Tunduma ili
kurahisisha shughuli za kibiashara na uzalishaji katika mji huo.
Prof. Mbarawa yupo
katika ziara ya kukagua miundombinu katika mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 Comments