Na Mwamvua
Mwinyi,Bagamoyo
Mbunge wa jimbo la
Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amesema kuna umuhimu wa kuandikwa historia na
ushiriki wa Wanabagamoyo katika makuzi na siasa ya hayati Mwl.Nyerere .
Amesema historia ya
Tanganyika kupata uhuru huwezi kutenganisha Uhuru wa watu wa Bagamoyo na maisha
ya baba wa Taifa kwani yapo aliyofanya akipitia Bagamoyo .
Alibainisha hayo
,wakati wa siku ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa aliyetutoka miaka
18 iliyopita ,ambapo chama cha mapinduzi (CCM)wilayani Bagamoyo kiliadhimisha
huko Lugoba .
Ridhiwani ambae
alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo ,alieleza Mwl .Nyerere aenziwe kwa
kuigwa kimatendo .
Alisema kwamba,wakati
akikumbukwa hayati Mwl.Nyerere ni vyema upendo,mshikamano na demokrasia
ikadumishwa miongoni mwetu .
Mwl.Nyerere aliwahi
kufunga kwa ajili ya kupigania uhuru wetu, na pia kuswali na baadhi ya mashehe
.
"Aliwahi kulala
,kuzungumza na kusali kata ya Mandela pale Mission akitokea Miono aliwahi
kwenda Mandela Msalabani ambako alikutana na kijana mmoja ambae alizungumza nae
ambapo kijana huyo ndie alikuwa dereva wake 1972-1980 " alisema Ridhiwani.
Nae mzee Mwalimu Akida
,ambae aliwahi kushuhudia mengi katika uongozi wa muasisi wa Taifa ,hayati
Mwl.Julius Nyerere ,aliwataka viongozi ndani ya CCM kuacha visasi na kuwekeana
chuki bali wafanyekazi kama timu moja ili kudumisha chama.
Aidha aliwasihi
kujenga tabia ya kuwafuata wanachama kuanzia kwenye mashina badala ya wanachama
kuwafuata wao maofisini ,;jambo litakalowasaidia kuzijua kero zinazowakabili na
kuweza kuzitafutia ufumbuzi
Mzee Akida alieleza
,uongozi ni dhamana na kioo cha jamii hivyo kila mmoja ajitambue na kuachana na
visasi na chuki ambazo zitachangia kudidimiza maendeleo ya chama .
Hata hivyo ,mzee Akida
alisema Mwl.Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa wa kupanga mambo ,alichukia
uhasama,ubaguzi ,ukabila,majungu ,rushwa na alipenda kutenda haki na kusisitiza
umoja .
,,:;Mwaka 1959 mie
nilimaliza shule pale Mwambao,mwaka 1962 nilikuwa idara ya mapokezi MANTEP na
pamoja na kufanya mazungumzo,alipokuja aliacha kitabu kinaitwa
TUJISAHIHISHE";
" Katika kitabu
hicho ukurasa wa kwanza kunaeleza umoja ambao ukidumishwa kutakuwa na mafanikio
,yawezekana kuna makosa tunayoyafanya na tofauti na watakavyoyafanya wengine
,ukimtilia mtu mashaka ,na anaekutilia mashaka ni jambo la kawaida"
"Hivyo msilipiane
visasi kwenye uongozi ni mwikoo,pendaneni,mkifanyiana visasi mtayumbisha mema
ambayo mmepanga kuyatekeleza kwa wananchi" alisisitiza mzee Akida .
Enzi za mwl.Nyerere
walisoma bure,kula bure na kupata ajira kirahisi sanjali na vitu vingine muhimu
bila kugharamia.
Mbunge wa viti maalum
Mkoani Pwani ,Subira Mgalu aliutaka uongozi wa CCM wilayani humo kufuatilia
utekelezaji wa ilani kwenye halmashauri za Bagamoyo na Chalinze kwa maslahi ya
wananchi .
Kwa upande wake
,mwenyekiti wa CCM Bagamoyo ,alhaj Abdul Sharif alielezea katika uongozi wake
hatopenda kuona mwanachama ama kiongozi mwenye chembechembe za chuki ,fitna na
majungu .
Alikemea makundi na
kuomba mshikamano baina yao pasipo kutengana.

0 Comments