Random Posts

Uhuru fm walipoliamsha dude jana kwenye viwanja vya mwembeyanga

 Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.

 Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere

 Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dula Makabila akiwa jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
 Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dula Makabila akiwapandisha mori mashabiki wake walioamua kupanda  jukwaani na kuonyesha uhodari wao wa kucheza muziki huo, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
 Dansa wa Dula Makabila akionyesha umahiri wake wa kucheza Singeli
 Vijana wa kundi la Mkubwa na Wanawe wakishambulia jukwani
 Msanii wa muziki wa Singeli akionyesha umahiri wake wa kuteka mashabiki
 Wachezaji wa timu zilizoshiriki kunogesha tamasha hilo wakichuana vikali kuwania mpira. 
 Wachezaji wa timu zilizoshiriki kunogesha tamasha hilo wakichuana vikali kuwania mpira.
 Mchuano mkali wa soka kwenye tamasha hilo
 Wanamuziki wa bendi ya TOT Plus wakishiriki kunogesha tamasha hilo. Kulia ni kiongozi wao Abdul Misambano
 Mcheza shoo wa TOT Plus Gabriel Romao maarufu kwa jina la Matukutuku akionyesha uwezo wake jukwaani
 Matukutuku wa TOT akicheza hadi kwa kichwa chini kukata kiu ya machabiki kwenye tamasha hilo
 KatamuTamu wa TOT Plus akionyesha uwezo wake wa kucheza shoo jukwaani.
 Mtangazaji wa Uhuru FM Kigwa akichangasha jukwaa.
 "Mashabiki piga keleeeee" Kigwa akihamasisha uchangamfu kabla ya Vijana Jazz kupanda jukwaani.
 Waimbaji wa Vijana Jazz wakiimba kwa hisia kali kudhihirisha kuwa muziki wa dansi bado una nafasi na mashabiki wake wapo.
 Kijana Saamata Hussein wa Vijana Jazz akionyesha umahiri wa 'kukaanga chips' jukwani.
 Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Dansi, Anna Mwaole akionyesha bado wamo, wakati akiimba na bdndi hiyo ya Vijana jazz. Anasema yeye ni Kongoro la supu lisiloisha utamu na pia ni kisu cha mgema
 Cosmas Adilian na Mohammed kandera wakionyesha umahili wa kupuliza tarumpeta katika bendi hiyo ya Vijana Jazz
 Shabiki akionesha 'kuguswa maisha yake' na burudani zilizokuwa zikimimika kutoka makundi mbalimbali kwenye tamasha hilo
 Mwimbaji wa Mwenge Jazz Shukuru Majaliwa akionyesha hisia zake wakati akiimba kibao cha siku nyingi cha Zena.
 Mwenge Jazz wakishambulia jukwaa
 Mwimbaji wa Mwenge Jazz akikoleza kwa kusakata muziki jukwaani
 Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akifurahia jambo na mwenzake wakati wa tamasha hilo, kabla ya kuanza utambulisho wa baadhi ya watangazaji wa kituo hicho cha radio. 

Post a Comment

0 Comments