Kaimu Katibu Mkuu wa
Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Anjelina Madete akimkabidhi Naibu Waziri wa Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano wa
Wizara hiyo Mhandisi Atashasta Nditiye nyaraka mbalimbali zinazosimamia
uendeshaji wa Sekta hiyo wakati wa kikao na Menejimenti ya Sekta hiyo
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Wizarani mjini Dodoma alipowasili kwa
mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika nyadhifa hiyo na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Naibu Waziri wa Sekta
ya Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa Menejimenti ya Sekta ya Mawasiliano wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ukumbi
wa mikutano Wizarani mjini Dodoma alipowasili kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe
kushika nyadhifa hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli
Mkurugenzi wa Idara ya
Rasilimali Watu na Utawala wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Bi. Kitolina Kippa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Sekta ya
Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara hiyo Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa
kikao na Menejimenti ya Sekta hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
Wizarani mjini Dodoma alipowasili kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika
nyadhifa hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli
Mkurugenzi wa Idara ya
Sera na Mipango wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano ndugu Sayi Katwale akitoa taarifa ya mikakati na mipango ya Sekta
hiyo kwa Naibu Waziri wa Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara hiyo
Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa kikao na Menejimenti ya Sekta hiyo
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Wizarani mjini Dodoma alipowasili kwa
mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika nyadhifa hiyo na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Hayo yameelezwa na
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa
kikao chake na Menejimenti ya Sekta ya Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo mjini
Dodoma mara baada ya kuwasili Wizarani
hapo kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kushika dhamana ya kuongoza Sekta
ya Uchukuzi na Mawasiliano ya Wizara hiyo.
Mheshimiwa Nditiye
amesema anawataka watumishi wa Sekta hiyo kuhakikisha kuwa wanafanyakazi kwa
bidii, weledi wa hali ya juu na uaminifu ili rasilimali za Taifa zinufaishe
wananchi na akaongeza kuwa “siko tayari kumvumilia mtumishi yeyote ambaye
atakwamisha utekelezaji wa majukumu ya Serikali”.
Ameitaka Menejimenti ya Sekta
ya Mawasiliano kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa za utekelezaji wa
majukumu ya Wizara ili wafahamu namna Serikali yao inavyowahudumia wananchi
wake. Amesisitiza kuwa utendaji kazi ukiwa mzuri, mapato ya Serikali
yanaongezeka na yataiwezesha Serikali kufikisha huduma mbalimbali kwa wananchi
wake.
Amewataka watumishi wa
Sekta hiyo kutambua, kuzingatia na kujipanga kutekeleza majukumu yao kwa
kulenga Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020, Mpango wa Miaka Mitano
wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2017-2021 na kauli za viongozi wakuu wa Serikali
ambazo ni maelekezo. Aidha, aliongeza kuwa ni muhimu kwa Sekta kushirikiana kwa
karibu sana na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu na wabunge
wote ili kuhakikisha kuwa Serikali inapokea maoni yao kwa kuwa wao ni
wawakilishi wa wananchi ili kuweza kuwahudumia wananchi hao.
Mhe. Nditiye
amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli kwa kumteua kwa kuwa wabunge wenye sifa na uwezo wako wengi ila
amemuamini na kumpa dhamana ya kumsaidia kuongoza Sekta hizo.
Pia, ameahidi
kwamba hatamuangusha Mhe. Rais Dkt. Magufuli na Waziri wake, Prof. Makame
Mbarawa na yuko tayari kutumikia wananchi kadri Mwenyezi Mungu atakavyopenda na
kumjalia. Vile vile amesisitiza kuwa kwa msaada wa watendaji wakuu na watumishi
wa Wizara ataweza endapo watampa ushirikiano wa kutosha.
Naye Kaimu Katibu Mkuu
wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Anjelina Madete amesema kuwa Menejimenti na watumishi wanamkaribisha na wako
tayari kumpa ushirikiano na hawatamuangisha ili wote kwa pamoja waweze
kutumikia wananchi kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Wakati akitoa taarifa
ya utekelezaji na majukumu ya Sekta hiyo kwa Mhe. Nditiye wakati wa kikao hicho,
Mhandisi Madete amesema kuwa Sekta imejenga miundombinu mbalimbali ya TEHAMA na
kuhakikisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini kwa kujenga Mkongo wa
Taifa wa Mawasiliano ambao unatoa huduma zake ndani na nje ya nchi, imejenga
Kituo cha Taifa cha Data, kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Anwani za Makazi na
Postikodi kwa kushirikiana na TAMISEMI, kufikisha huduma za mawasiliano
vijijini kwa kuzipatia kampuni za simu ruzuku na kujenga minara, kuwezesha
upatikanaji wa huduma mtandao kwa taasisi za Serikali na sekta binafsi na uwepo
wa mifumo ya kielektroniki ambayo imeiwezesha Serikali kuongeza makusanyo ya
kodi na mapato yake kwa ufanisi na kwa wakati hivyo kupunguza mianya ya rushwa
na upotevu wa mapato ya Serikali.
Katika hatua nyingine, Mhandisi Madete
amempatia Mhe. Nditiye nyaraka mbalimbali zinazosimamia sekta ya Mawasiliano
ikiwemo Sera, sheria na kanuni, Mpango Mkakati na hotuba ya Bajeti ya mwaka wa
fedha wa 2017/2018.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano




0 Comments