Mafundi
wakiendelea na ukarabati wa meli ya Mv. Clarius leo katika Bandari ya Mwanza.
Kukamilika kwa ukarabati wa Meli hiyo inayotoa huduma katika visiwa vilivyo
katika ziwa Victoria kutarudisha huduma za usafirishaji na abiria katika visiwa
hivyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mbele), akitoka
kuangalia ukarabati wa meli ya Mv. Clarius, katika Bandari ya Mwanza,
leo. Meli hiyo inatoa huduma katika visiwa vilivyo kwenye ziwa Victoria.
Muonekano
wa Meli ya Mv. Umoja yenye uwezo wa kubeba behewa 22. Meli hiyo inasafirisha
mizigo kutoka Bandari ya Mwanza kuelekea Bandari ya “Port Bell” Uganda.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa nne kulia),
akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Xavier
Kapinga, alipofika Bandari ya Mwanza leo kujionea maendeleo ya ukarabati wa
meli ya MV. Clarias katika Bandari hiyo.
Mhandisi
Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Xavier Kapinga, akifafanua jambo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu
Kushoto mbele) wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati wa meli katika Bandari
ya Mwanza, Leo.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi, akimuonesha Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia), hatua
zilizofikiwa za ukarabati wa meli ya Mv. Clarius na Mv. Umoja katika Bandari ya
Mwanza.
......
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amekagua eneo
lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na yakisasa itakayotoa huduma za
usafirishaji katika Ziwa Victoria.
Akizungumza
na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Profesa Mbarawa, amewataka
wafanyakazi wa Kampuni hiyo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi ili kazi hiyo
ianze mara moja na kukamilika kwa wakati.
“Mkandarasi
ameshapatikana hivyo hakikisheni mnatoa ushirikiano na mnafanya uhakiki wa
kimahesabu vizuri ili kazi hii ifanyike kwa gharama nafuu, ubora na muda
mfupi”, amesema Profesa Mbarawa.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mbarawa, amekagua maendeleo ya ukarabati wa meli ya Mv.
Clarias na Mv. Umoja ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na hatua zilizofikiwa,
na hivyo kuwataka MSCL kutafuta mizigo ya kusafirisha kutoka Bandari ya Mwanza
kwenda Bandari ya “Port Bell”, nchini Uganda.
“Kukamilika
kwa meli kuwiane na kasi ya kutafuta mzigo mwingi ili meli hizi zifanye
biashara wakati wote na kuhakikisha Kampuni yenu inapata mapato mengi yatakayowawezesha
kujiendesha kwa faida”, amesisitiza Waziri Mbarawa
Naye,
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi,
amemhakikishia Profesa Mbarawa, kuwa wamejipanga kufanya ukarabati mkubwa wa
meli za Mv. Victoria, Butiama na Liemba ili kuziwezesha meli hizo kufanya kazi
katika ubora wake wa awali na kupunguza tatizo la usafiri katika ziwa Victoria
na Tanganyika.
“Tumeweka
mkakati wa kuhakikisha tunazikarabati meli zetu zote ili ziwe katika ubora
unaostahili wakati wote”, amefafanua Bw. Hamissi.
Katika
kuhakikisha maendeleo ya kibiashara na kuichumi yanafikiwa katika Ukanda
wa maziwa makuu nchini, Serikali imejipanga kuhakikisha inafufua usafiri
wa meli za abiri na mizigo katika ukanda huo.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.






0 Comments