Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali
Hassan Mwinyi akiwapungia mkono wazee wakati wakiingia kwa maandamano
kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere
Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana
akitoa salamu za Mkoa kwa Mgeni Rasmi wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Sera ya Taifa
ya Wazee ya Mwaka 2003 kwa Mgeni wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee nchini Mzee Sebastian
Bulegi akisoma hotuba kwa niaba ya Wazee nchini wakati wa maadhimisho ya Siku
ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017 .
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali
Hassan Mwinyi akizungumza na wazee wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee
Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017 .
Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan
Mwinyi (hayupo Pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika
katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali
Hassan Mwinyi akiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa na wazee katika moja ya
banda la Maonesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika
katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akitoa zawadi kwa mmoja wa wazee wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
..................
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
Vijana nchini wameshauriwa kujitolea na kuwatunza wazee katika maeneo yao
ili kupata ushauri na busara za wazee hao kwa maendeleo yao na taifa.
Hayo yamesemwa Mjini Dodoma na Rais Mstaafu wa
Awamu ya Pili Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi alipokuwa akizungumza na wazee
katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kila
Oktoba Mosi ya kila mwaka.
Mhe. Mwinyi amesema kuwa jukumu la kuwatunza na
kuwalea wazee sio la Serikali pekee bali jamii pia ina nafasi yake katika kuwatunza wazee
hasa Vijana.
Mhe. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali imejitaidi
sana kuweka mazingira mazuri kwa wazee kwa kuwapatia huduma za Afya na
kuwatunza wazee wote ambao hawana ndugu wa kuwatunza katika makambi mbalimbali
ya wazee nchini.
“Niwaombe vijana mtutunze sisi wazee kwani na sisi
tulikuwa vijana kama ninyi na mkiweka utamaduni huu utawasaidia na ninyi mkiwa
wazee hapo baadae” alisema Mhe. Mwinyi.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, MAendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Mstaafu
Mhe. Mwinyi kuwa Serikali itaendelea kuwatunza wazee nchini na kuhakikisha wanapata hudumu zote muhimu.
“Nikuhakikishie Mhe. Mwinyi kuwa tutaendelea
kuwatunza wazee kwa kuwapatia huduma muhimu hasa huduma za Afya” alisema Mhe.
Ummy.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee nchini Mzee Sebastian
Bulegi amemuomba Mhe. Mwinyi kufikisha shukurani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa moyo wake wa kuwajali wazee nchini.
“Mhe. Mwinyi naomba utufikishie shukurani zetu kwa
Mhe.Rais Magufuli kwa kutujali wazee hasa kwa kutatua changamoto zetu
zinazotukabili” alisema Mzee Sebastian.
Siku ya Wazee Duniani huadhimishwa Oktoba Mosi kila mwaka kufuatia
Azimio la Umoja wa Mataifa linalozitaka nchi wanachama kutenga siku maalumu ya
kutafakari mchango wa Wazee katika maendeleo ya jamii na kuwaenzi ili wawe na maisha bora na yenye matumaini na Kauli
mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “
Kuelekea uchumi wa Viwanda:Tuthamini Mchango, Uzoefu na Ushiriki wa Wazee kwa
maendeleo ya Taifa”.









0 Comments