Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani
akimkabidhi Ofisi Waziri wa Madini, Angellah Kairuki. Wanaoshuhudia katikati ni
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, kulia kwaDkt. Kalemani ni Naibu Waziri
wa Nishati Subira Mgalu na wa kwanza kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Prof. James
Mdoe.
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani
(kulia aliyekaa) Waziri wa Madini Angellah Kairuki kushoto(aliyekaa) wakiweka
saini Nyaraka za Makabidhiano ya Wizara. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa
Madini Stanslaus Nyongo , Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Kaimu Katibu
Mkuu Prof. James Mdoe (wa kushoto).
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani
(katikati mbele), Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati mbele), Naibu
Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kushoto) Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo (Kushoto kwa Waziri Angellah Naibu Waziri wa Nishati, Katibu Mkuu Prof.
James Mdoe wakifuatilia kikao kati ya viongozi hao na Wajumbe wa Menejimenti wa
iliyokua Wizara ya Nishati na Madini.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (aliyesimama)
akieleza jambo wakati wa kikao kati ya vingozi hao na Menejimenti ya iliyokuwa
Wizara ya Nishati na Madini.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini
Dkt. Medard Kalemani amemkabidhi Ofisi Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.
Walioshuhudia Makabidhiano hayo ni Naibu Waziri wa Nishati Subira
Mgalu, Naibu Waziri Wa Madini, Stanslaus Nyongo, Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara za Nishati na Madini, Prof. James Mdoe na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Vilevile, Dkt. Kalemani ametumia fursa hiyo
kuwaaga na kuwashukuru kwa ushirikiano waliompa waliokuwa Watumishi wa
iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Dkt. Kalemani
amempongeza Kairuki kwa kuchaguliwa kwake kuwa Waziri wa kwanza Mwanamke wa
Wizara ya Madini na kumweleza kuwa, Watanzania wana matumaini makubwa na
mabadiliko ya Wizara na kuongeza kuwa, pamoja na majukumu mengine analo jukumu
la kuhakikisha anaendeleza mikakati ya Serikali ya kuendeleza uanzishwaji
migodi mipya hususan ya madini ya viwandani kama Graphite.
Naye Waziri Kairuki amesisitiza suala la ushirikiano kwa
watumishi wa Wizara husika ili hatimaye kuwezesha sekta husika kuwa na mchango
zaidi kwa taifa na hatimaye watanzania
waweze kunufaika zaidi na Rasilimali hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo
amesema kuwa viongozi wa wizara husika wanao wajibu wa kuonesha mchango wa
madini katika pato la Taifa hivyo amesisitiza uwepo wa ushirikiano kati ya
Viongozi na Watumishi wa Wizara ili wajibu huo utekelezwe.
0 Comments