Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto,
Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na wakuu wa Idara na vitengo
mbalimbali hawapo pichani wa Wizara ya
afya kuhusiana na kuimarisha huduma bora za afya nchini leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto
ni Naibu wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndungulile na wa kwanza kulia ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. Wakati wa kikao chake na wakuu
hao.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa
kwanza kushoto akiongea na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali wa Wizara ya
afya hawapo pichani kuhusiana na kuimarisha huduma bora za afya nchini leo jijini Dar es salaam, katikati ni Waziri
wa Wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu na kulia ni Katibu Mkuu Wa Wizara ya Afya Dkt.
Mpoki Ulisubisya. Alipokutana na wakuu hao.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya
afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia kwa makini
maelezo kutoka kwa Waziri mwenye dhamani hiyo
Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile hawapo
pichani wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya,
Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakimpongeza Naibu Waziri wa Wizara
hiyo Dkt. Faustine Ndungulile hayupo pichani mara baada ya kuwapa maelezo
wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo katika ofisi ndogo za wizara jijini
Dar es salaam.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya
afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia kwa makini
maelezo kutoka kwa Waziri mwenye dhamani hiyo
Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile hawapo
pichani wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto,
Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia akiteta jambo na Naibu wake Dkt. Faustine
Ndungulile kushoto mara baada ya kikao
na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
WIZARA ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
watoto imejidhatiti kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto mpaka kufikia
2020 ili kutokomeza vifo vya wajawazito na watoto wachanga .
Hayo yamesemwa na Waziri wa afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati
alipokutana na Wakuu wa Idara na vitengo Mbalimbali kwa ajili ya utambulisho wa
Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndungulile katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
salaam.
“Vifo vya wajawazito vimekua tishio nchini hivyo
ni lazima tuimarishe huduma za afya ya mama na mtoto ili tufikie malengo ya
kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi mpaka kufikia 2020 ili kujenga taifa lenye
watu wenye afya bora” alisema Waziri ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa katika kuboresha
hilo amewaagiza wakuu wa idara wizara ya afya kushirikiana na mfuko wa bima ya
afya nchini(NHIF) kuona kama kuna uwezekano wa kuanzisha bima ya afya kwa
wajawazito kwa bei nafuu hadi kufikia Julai mosi 2018.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa
wanamipangilio ya kutokomeza kabisa tatizo la dawa nchini kwa kuweka mpango
mkakati kati ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na vituo vitoavyo huduma za afya ili kuepuka tatizo hilo lisijirudie mara kwa
mara .
Kwa upande wake Naibu Waziri Dkt. Faustine
Ndungulile amesema kuwa ameshukuru kwa kupewa dhamana hiyo na atashirikiana
vyema na Waziri pamoja na watendaji wa Wizara hiyo ili kuleta ufanisi na Huduma
bora za afya nchini.
“Nitashirikiana na Waziri wangu pamoja na nyinyi
watendaji wenzangu katika kusimamia na kutekeleza sera ya afya ili kuweza kutoa
huduma bora za afya kwa watanzania wote bila ya kujali rika,jinsia wala umri”
alisema Dkt. Ndungulile
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya
amesema kuwa wamepokea maagizo hayo amabayo baadhi wameanza kuyatekeleza na mengine atawahimiza watendaji wake kuendana na kasi
ya awamu ya tano ya HAPA KAZI TU ili kuifikisha nchi katika afya bora.








0 Comments