Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu.
Na WAMJWW
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu aagiza Hospitali,
na Vituo vya Afya vyote vya Serikali nchini kuanzia leo October 26 kutoa huduma
ya uchunguzi wa Saratani kila siku wakati wa kliniki ya mama na mtoto, sambamba
na huduma hizi, kila mwezi vyatakiwa kuwa na siku moja kwaajili ya kuchunguza
na kufanya matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya
matiti.
Ameyasema hayo wakati
alipofungua matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti,
yalifunguliwa katika viwanja vya
hospitali ya Ocean Road mapema leo jijini Dar es salaam.
Aidha Mh. Ummy
ameipongeza kazi nzuri inayofanywa na Uongozi wa Hospitali ya Ocean Road katika
kutimiza majukumu yake ikiwemo kuongeza vitanda
40 mpaka vitanda 100 kwa gharama
zao kwaajili ya wagonjwa wa saratani pindi wanapopata huduma za matibabu ya
Chemotherapy.
?Katika kuwaunga mkono
Serikali ya awamu ya tano ya Mh. Magufuli imewapatia Bilioni 5 kwajili
yakukamilisha mashine za kisasa za matibabu ya Saratani kwa kutumia mionzi.?
Alisema Mh. Ummy Mwalimu
Aidha Mh. Ummy Mwalimu
ametoa maelekezo kwa Uongozi wa Hospitali ya Ocean Road kuwa wanatakiwa kwenda
kwenye shule za Msingi na Sekondari ili kuwajengea watoto uelewa kuhusu ugonjwa
wa Saratani, lakini ni vipi wataweza
kujikinga na magonjwa yasiyo yakuambulizwa ikiwemo ugonjwa wa Saratani.
Pia Mh. Ummy alitoa
rai kwa wananchi wote hususani wanawake kujitokeza kupima ugonjwa huo kwani
unatibika endapo itagunduliwa mapema,
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Grace Maghembe ambae
pia alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam , ameipongeza Serikali ya awamu
ya tano chini ya Raisi Dkt. John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto kwa kazi kubwa wanayoifanya ikiwemo
kuongeza kwa bajeti ya Dawa , vifaa tiba vya uchunguzi na matibabu.
Kwa upande mwingine
Dkt. Grace Maghembe kwa niaba ya bodi ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu na bidii kubwa katika kuhakikisha
kwamba wanakabiliana na ugonjwa huu wa Saratani kwa wananchi hasa wale wa hali
ya chini na kuahidi kuendelea kuboresha huduma hii.
?Niwaombe wananchi wa
Mkoa wa Dar es salaam kwenda kupima Saratani kwani ni bure, usisubiri mpaka
kuugua, ukichelewa grarama zinaongezeka lakini pia uwezekano wa kupona unakuwa
ni mdogo?. Alisema Dkt Grace Maghembe
Aidha Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amemhakikishia Mh.
Ummy Mwalimu kwamba upatikanaji wa dawa katika Hospitali hiyo ni 80% na dawa za
wagonjwa wengi zinapatikana kwa 100%, ukilinganisha na 2015/2016 upatikanaji wa dawa ilikuwa 4%
tu, jambo ambalo lilikuwa ni changamoto
kubwa na kufanya malalamiko ya dawa kuwa makubwa sana katika hospitali hiyo,
hivyo kuishukuru Serikali ya Magufuli kwa niaba ya Waziri wa Afya Mh. Ummy
Mwalimu.
Mwisho Dkt. Julius
Mwaiselage amemhakikishia Mh. Waziri kwamba Hospitali ya Ocean Road ipo katika
hatua ya Mwisho ya kuweka mashine mpya mbili (Linear accerelators), hivyo
zitasaidia kupunguza muda wa kusubiri kwa wagonjwa kusubiri huduma , lakini
kubwa kupunguza wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi.

0 Comments