Random Posts

Waziri wa ujenzi Prof. Makame Mbarawa ameigiza Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo kuwachukulia hatua kali wataalam wote watakaobainika kupokea au kutoa rushwa.

 Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa  akifungua mkutano wa 28 wa wadau wa bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji wa majenzi  wa siku mbili katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam Oktoba 12-13 2017, lengo la mkutano huo ni kujifunza mambo mapya yanayotokea katika utendaji sekta ya ujenzi. 
 Waandishi wa habari wakiwa kazini.
 Wadau wa bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji wa majenzi  wakiwa katika mkutano wa siku mbili katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam Oktoba 12-13 2017, lengo la mkutano huo ni kujifunza mambo mapya yanayotokea katika utendaji sekta ya ujenzi.
 Kaimu Msajili  wa bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi Albert Munuo akielezea  mpango wa mafunzo endelevu wakati wa mkutano wa siku mbili katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam Oktoba 12-13 2017, lengo la mkutano huo ni kujifunza mambo mapya yanayotokea katika utendaji sekta ya ujenzi.
 Mashaka Mbundala akifafanua jambo
 Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa  bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji wa Majenzi, Ezekiel Stephen (katikati) akiwa pamoja na wadau wengine wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo.
 Wadau wakiwa kwenye mkutano.

 Afisa Masoko wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania, Bi Irene Mwakapugi (kushoto) akielezea utengenezaji dari kwa kutumia chuma badala ya mbao (kulia) Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Rachel Zhong.
 Wadau mbalimbali wakijiandikisha kabla ya kuingia ukumbini.
Watumishi wa bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji wa Majenzi.
  Kaimu Msajili wa bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi Albert Munuo (aliyeweka mkono mfukoni) akisikiliza jambo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo DKT.Ambwene Mwakyusa.
 Muonekano wa mabanda katika mkutano wa siku mbili katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam Oktoba 12-13 2017, 
 Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akipewa maelezo kutoka mmoja wa wadau wabunifu majengo na wakadiriaji wa majenzi alipotembelea mabada mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam Oktoba 12-13 2017, 
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji wa majenzi  wa siku mbili katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam Oktoba 12-13 2017, lengo la mkutano huo ni kujifunza mambo mapya yanayotokea katika utendaji sekta ya ujenzi. 

..

Na Mwandishi wetu

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa  ameiagiza bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji wa majenzi kuwafutia usajili na kuwachukulia hatua kali wataalam wote watakaobainika kupokea au kutoa rushwa katika kutekeleza wajibu wao.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika ufunguzi wa mkutano wa 28 wa wadau wa bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji wa majenzi  amesema kuwa ni muhimu kwa bodi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika miradi ili kubaini wale wote wanaukiuka taratibu kwaajili ya rushwa.

Waziri MBARAWA ameipongeza bodi hiyo kukutanisha wataalam hao  na wadau wa bodi ya nchini Kenya na kuwaasa kuendelea kukutana kubadilishana ujuzi kwakuwa teknolojia inakua kwa kasi sana hivyo ni vema kujifunza zaidi ili kukabiliana na majanga ya matetemeko ya ardhi.

Pia ameipongeza bodi hiyo kwa kubuni michoro  ya majengo kwa gharama nafuu na kusema kuwa itawanufaisha  watanzania katika kutatua matatizo ya ujenzi.

Aidha Profesa MBARAWA ametoa agizo kwa wakurugenzi na watendaji wa makampuni ya sekta ya ujenzi  kuhakikisha vijana wanapewa fursa ya kuwekwa katika kila sehemu yenye miradi mkubwa  ili waweze kujifunza na kunufaika kupitia miradi hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Msajili wa bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi ALBERT MUNUO amesema kuwa semina hiyo ni mwendelezo wa mpango wa mafunzo endelevu ambazo bodi imekuwa  ikiandaa kwa lengo la  kuwakutanisha wabunifu wa majengo,wakadiriaji majenzi na wataalam wanaohusiana na sekta ya ujenzi lengo likiwa kujifunza mambo mapya yanayotokea katika utendaji kazi.

Mkutano huo wa bodi  umewakutanisha wadau na wataalamu wa majenzi na makandarasi mada kuu ni mbinu ya kupunguza madhara ya matetemeko ya ardhi,ukaguzi wa miradi ya ujenzi na matengenezo ya majengo na miundombinu.

Post a Comment

0 Comments