Katibu Mkuu
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akiongea na
watumishi wa Wizara hiyo mjini Dodoma ambapo amewataka kufanyakazi kwa
uadilifu kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma. Wa kwanza kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Nicholaus William.
Katibu Mkuu
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akiongea na
watumishi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi Mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri
Mangi, WHUSM-Dodoma).
....
Na Eleuteri Mangi,
WHUSM-Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi amewataka watumishi wa wizara
hiyo kufanyakazi kwa uadilifu na weledi kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa
Umma katika kuwahudumia wananchi.
Katibu Mkuu Bi.Suzan
amesema hayo mjini Dodoma katika kikao na watumishi wa Wizara ambapo amewahamasisha
kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwatumikia wananchi
kupitia sekta za wizara hiyo ambazo ni Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
“Endeleeni kuwa
waadilifu na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, ni wajibu wa kila mmoja
wetu kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Sheria zipo ili zitekelezwe”
alisisitiza Katibu Mkuu Mlawi.
Aidha, Katibu Mkuu huyo
amewataka watumishi hao kushirikiana kwa karibu na viongozi ili kuimarisha
umoja utakaoleta maarifa na ufanisi wa matokeo bora ya kiutendaji kwa manufaa
ya umma.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Nicholaus
William amewaomba watumishi kuzingatia kufika ofisini kwa muda uliopangwa na
kuwahudumia wananchi ipasavyo ili kujenga taifa lenye matokeo chanya ya
kiutendaji na hivyo kuleta maendeleo katika Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya
watumishi, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo amewahakikishia
kuwapa ushirikiano viongozi hao kwa kufanya kazi kwa kujituma ili
kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Wizara.
“Tutafanyakazi kwa
uadilifu kwa mujibu wa Sheria, kanuni, taratibu na maelekezo yenu kwa kufuata
kasi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
tukiongozwa na Sera yake ya “Hapa Kazi Tu”.


0 Comments