Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na
kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipoziikwa mwanaye
ili kwenda kumzika upya.
Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu
kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye
alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea
kifo cha muigizaji huyo.
“Kwa sasa sina la kusema ila naishukuru sana Mahakama
kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka
hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba”.
Mama Kanumba
Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi
kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa
mteja wake.
Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya
kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi
wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012
Chanzo:thechoicetz

0 Comments