Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akimtunuku Shahada ya Uzamivu katika Uchumi Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba katika mahafali ya 47
ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandara.
Wahitimu wa Shahada ya Sayansi ya Uzamili Katika masuala ya
Jiolojia wakifurahia mara baada ya kutunukiwa rasmi shahada hiiyo katika
Mahafali ya 47 ya chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza
Mukandara akitoa neno la shukrani mara baada ya zoezi la kuwatunuku
degree zao wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya wahitimu wakiwa katika nyuso za furaha kufuatia
kuhitimu masomo yao kama walivyokutwa na mpiga picha wetu katika
mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.
Lameck Mwigulu Nchemba mara baada walipokutana katika mahafali ya 47 ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam. Mwigulu Nchemba
nimiongoni mwa wahitimu waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Uchumi
katika mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika Mlimani City.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali
waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Mahafali ya 47 ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamala ya
Usimaizi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isack.
(Picha
na MAELEZO)






0 Comments